KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Morogoro, limewataka wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa
hilo kuacha kuvaa mavazi yanayoonyesha maungo yao hususan matiti na
migongo ili kuepuka kuwakwaza wachungaji.
Akihubiri wakati wa misa maalumu ya harambee ya kuchangia ujenzi wa
kanisa hilo usharika wa Kilakala iliyoongozwa na Waziri Mkuu
aliyejiuzulu, Edward Lowassa, msaidizi wa Askofu katika dayosisi
hiyo, George Pindua, alisema kuwa baadhi ya wanawake wanaokwenda kufunga
ndoa huvaa nguo zisizo na heshima.
“Nyie wanaume ambao mmepanga kufunga ndoa na wake zenu hakikisheni
mnawanunulia nguo zenye heshima, atakayekuja na nguo zinazoonyesha
matiti au mgongo hatutamfungisha ndoa,’’ alisema.
Alisema kuwa kina mama wa kanisa hilo wanapaswa kuandaa vitenge vya
kuwafunika wanawake wanaovaa nguo zisizo na maadili ili kuepusha kanisa
kupata aibu.
Naye Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob ole Mameo, alisema
kuwa wamekuwa wakitoa mahubiri mema ili kuhakikisha waumini wao
wanadumisha amani na utulivu.
Alisema kuwa taifa hili limejengwa katika misingi ya kudumisha amani na utulivu hivyo kila muumini anapaswa kuilinda isipotee.
No comments:
Post a Comment