BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Utamu’ inayofanya vizuri 
katika vituo mbalimbali vya redio na runinga, nyota wa muziki wa kizazi 
kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, anajipanga kuachia ngoma yake 
mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mapenzi ni Sumu’.

                                                         Abdul Sykes ‘Dully Sykes’
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dully alisema
 ndani ya kibao hicho ipo sauti ya mkali wa muziki huo, Ambwene Yesaya 
‘AY’, pamoja na mwanadada Jokate Mwegelo.
Alisema yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, 
ambacho anaamini atakiachia pamoja na video yake mwanzoni mwa Februari.
“Namshukuru Mungu kazi zangu huwa zinapokewa vizuri na mashabiki 
wangu, kitu ambacho kinanipa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika 
‘game’ hivyo nawaomba mashabiki wa kazi zangu waendelee kusubiri vitu 
vizuri kutoka kwangu,” alisema Dully.
  Aliongeza kuwa ameamua kumshirikisha AY katika kazi hiyo kutokana na 
uwezo wake katika tasnia ya muziki, ikiwa ni pamoja na historia yake 
nzuri ya kuutangaza muziki wa Bongo katika mataifa mbalimbali. 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment