MEYA wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Jerry Silaa ametakiwa kutoa
ufafanuzi juu ya sh milioni 100 zilizotengwa kwa ajili ya matengezo ya
barabara katika bajeti ya 2011/2012.
Jerry Silaa
Hayo yalisemwa na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara waliouandaa.
Hayo yalisemwa na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara waliouandaa.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu wa Jimbo la Ukonga, Juma
Mwaipopo, alisema kuwa fedha hizo zilizotengwa na Halmashauri ya Ilala
katika kipindi hicho hadi sasa hazijafahamika zimefanyiwa nini.
Alisema kuwa halmashauri ilitenga sh bilioni 93 kwa matumizi ya jimbo
hilo, zikiwemo sh milioni 100 kwa kata sita ambazo zingetumika kwa
ajili ya upanuzi na matengenezo ya barabara pamoja na kusambaza huduma
ya maji kwa wananchi, jambo ambalo limekuwa ni kitendawili.
Alisema kuwa eneo hilo kijiografia lina wakazi wengi, lakini wachache
wao ndio waliounganishwa na huduma ya maji safi kutoka bomba la Mto
Ruvu, huku baadhi wakitumia maji ya visima na wengine kununua katika
magari yanayosambaza huduma hiyo.
“Tunahitaji kuwa na maamuzi ya pamoja juu ya Silaa, kwa sababu
hatujui tumetoka wapi wala tunaelekea wapi hadi sasa? Inawezekana hajui
kazi yake kwa sababu hatuna maendeleo wala mabadiliko katika kata
yetu, Watanzania tudai haki ambazo serikali ilituahidi itazitekeleza
bure” alisema Mwaipopo.
Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Silaa alisema fedha hizo ziko chini
ya Mkurugenzi wa halmashauri, na zitatolewa kwa utaratibu baada ya
kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
No comments:
Post a Comment