ALIYEKUWA mshiriki wa shindano la Maisha Plus 2012, Rashid 
Ndunduke, amefariki dunia kijijini kwao juzi baada ya kuvamiwa na 
kiboko.
Rashid ambaye kwenye shindano hilo la Maisha Plus alikuwa akiwakilisha
 Mkoa wa Lindi, alikuwa kivutio kwa watazamaji wengi, hasa kwa mambo 
mbalimbali aliyokuwa akifanya ndani ya kijiji hicho, ikiwamo kuonesha 
maisha halisia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kaka wa marehemu, Hassan 
Ndunduke, mdogo wake alikutwa na mauti akiwa anavua samaki, ghafla 
kiboko alimvamia na kumjeruhi.
  Hassan alisema licha ya juhudi za hospitali ya jirani huko kijijini kwao Njinjo kuokoa maisha yake zilishindikana.
Marehemu alijiunga Maisha Plus kama mmoja wa wawakilishi wa Mkoa wa 
LindiAkiwa kijijini Maisha Plus, alifahamika kwa wengi kama Nanjilinji, 
Master Key au Baba Sampo.
  Shughuli alizozifanya Maisha Plus ni pamoja na kuuza duka, uchongaji 
na kuna wakati aliwahi kuongoza kwa kuwa na fedha nyingi zaidi 
ikilinganishwa na wanakijiji wenzake, sambamba na uhodari wa kukwea miti
 mirefu
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment