MBUNGE wa Iramba Magharibi kupitia CCM,
Mwiguli Nchemba, amesema atapeleka hoja binafsi katika kikao cha Bunge
lijalo kuitaka Serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria, wa
kuanzisha Mfuko wa Elimu ya Juu.
“Serikali ina mzigo wa kugharimia elimu ya juu kwa bajeti ya Serikali inayoumiza idara zingine za wizara kwa mfano, takribani asilimia 80 ya matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2012/13 ilielekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu,”alisema Nchemba.
Alisema mfuko huo utasaidia kuwa na vyanzo vya
uhakika vya mapato na mfumo wa kukopesha wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia
taasisi za kibenki na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii zitakazowezesha
kumkopesha kila mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu
kwa asilimia 100.
“Msingi wa hoja yangu ni madhara yanayojitokeza kutokana na mfumo wa utoaji wa mikopo unakwamisha nia njema ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya kutoa elimu ya juu kwa Watanzania wengi hususan watoto wa maskini.”alisema.
Nchemba alitoa mfano kwamba takwimu zinaonyesha
mwaka 2004/05 zilitumika zaidi ya Sh22 bilioni kwa ajili ya wanafunzi
16,345 kwa kiwango cha Sh2,500 kwa siku, mwaka 2005/06 kwa wanafunzi
42,729 zilitumika takribani Sh56 bilioni.
Alisema mwaka 2011/12 zilitumika takribani Sh320
bilioni kwa ajili ya wanafunzi 94,073 kwa kiwango cha Sh7,500 kwa siku
na kwamba ifikapo mwaka 2015/16 tutahitaji zaidi Sh500 bilioni kwa
wanafunzi 140,000 kitu ambacho kinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi.
“Wizara zinazosimamia moja kwa moja Rasilimali za Taifa mfano Maliasili na Utalii, Nishati na
“Wizara zinazosimamia moja kwa moja Rasilimali za Taifa mfano Maliasili na Utalii, Nishati na
Madini, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mifugo na Uvuvi zipangiwe kiwango cha fedha za kuchangia kwenye mfuko wa elimu ya juu kila mwaka ili kusaidia kutunisha mfuko huo.”alisema na kuongeza;
“Mikopo yote itozwe riba na kiwango cha riba kiwe
sawa gharama ya ukopaji kwa Serikali. Hii itasaidia kulinda thamani ya
mkopo na kusaidia mkopo usiolipwa kuongezeka kwa kiwango sawa na kile
cha uuzaji wa dhamana za Serikali.”
No comments:
Post a Comment