WIKI moja baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao (CHADEMA)
kuzindua kikundi cha wanawake cha Mafuruto, wanawake hao wameanza
kunufaika na mkopo kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.
Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao (CHADEMA).
Akitoa mkopo kwa wanawake hao, mwanzoni mwa mwaka huu, mbunge huyo
alisema anataka kuwa tofauti na wanasiasa wengine ambao huishia kuahidi
na kupotea bila kutekeleza ahadi.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha wanawake waweze
kujitegemea na kuachana na tabia ya kusubiri wakati wa kampeni na kupewa
vitenge kama kishawishi cha kupiga kura.
“Hii tabia ya kusubiri vitenge kwenye kampeni iishe kwa sababu mtakuwa mna uwezo wa kujitegemea,” alisema.
Abwao alisema kuwahadaa wanawake ni kuyumbisha maendeleo kwa kuwa wanawake wana mchango mkubwa wa kuleta maendeleo kwa taifa.
Hata hivyo, alisema nchi inakosa viongozi bora kwa sababu ya watu wenye pesa wanawatumia maskini kuwahonga, ili wawachague.
Naye Katibu Mtendaji wa kikundi hicho, Yusta Udamwa, alisema endapo
taifa litatambua mchango wa wanawake, uchumi utasonga mbele.
Mwisho
No comments:
Post a Comment