EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, January 3, 2013

Viongozi wa dini wapinga Serikali kusafirisha gesi

MGOGORO wa gesi umeingia sura mpya, baada ya viongozi wa dini mkoani Mtwara kuungana na wananchi kupinga usafirishwaji wake kwenda Dar es Salaam, huku Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akitoa ufafanuzi wa faida za mradi huo kwa taifa.
 
Mbali na ufafanuzi huo, Waziri Muhongo amemlipua Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji kwa msimamo wake wa kuungana na wananchi hao, akieleza kuwa hamwelewi kwa kuwa wabunge akiwamo yeye, walishirikishwa vilivyo kwenye mradi huo na kulipwa posho lukuki.


Viongozi wa dini waliojitosa kwenye mgogoro huo ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Newala, Oscar Mnung’a na Askofu Mteule wa Kanisa la KKKT, Dayosisi Mpya ya Kusini Mashariki, Mchungaji Lucas Mbedule.

Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamepinga mradi wa kusafirisha nishati hiyo kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa hawaoni ni namna gani utawanufaisha wakazi wa Mtwara.
Askofu Mnung’a alisema anapingana na uamuzi wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na badala yake kuishauri Serikali ijenge mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara.

“Lazima wananchi wa Mtwara waamke, tumejifunza kule Songosongo, gesi imekwenda Dar es Salaam, si Kilwa wala Lindi iliyofaidika na gesi ile… gesi ibaki Mtwara, mikoa ya kusini iimarishwe,” alisema Askofu Mnung’a na kuongeza:

“Hii yote ni Tanzania, hakuna ubaya wowote ile mitambo ya kufua umeme ikawekwa Mtwara… wafikirie leo hatuombei ila watu wakilipua Kidatu (Morogoro), nchi itakuwa gizani, lazima tutawanye rasilimali zetu siyo kila kitu Dar es Salaam.”
Askofu huyo alimpongeza Murji kwa kuweka wazi msimamo wake kuhusu suala hilo na kumshangaa Mbunge wa Masasi Mariam Kasembe anayeunga mkono akisema, mbunge huyo hawakilishi maoni ya wananchi.

“Nimewaambia waumini wangu kuwa tuwe tayari kutetea rasilimali yetu…. nampongeza Murji kwa kutetea masilahi ya wananchi,” alisema Askofu Mnung’a.
Askofu Mbedule alisema hapingi gesi kwenda Dar es Salaam ila hadi pale ahadi za Serikali zitakapotimizwa kwa wananchi wa Mtwara.
 

“Kwenye salamu zangu za Krismasi niliwaambia waumini kuwa ni wakati wa kuidai Serikali kutimiza ahadi zake kwa wananchi… wananchi wa Mtwara waliahidiwa viwanda, hakuna kiwanda hata kimoja, gesi inaondoka... hapana sikubaliani nalo,” alisema Mchungaji Mbedule na kuongeza:

“Serikali itueleze bomba la gesi kwenda Dar es Salaam litatoa ajira ngapi kwa wananchi wa Mtwara? Hilo moja, pili bomba hilo litachochea vipi uwekezaji kwa mikoa ya kusini… kama hakuna majibu ya hayo basi mimi nazuia gesi isiende Dar es Salaam.”
Alisema Rais Jakaya Kikwete aliwaahidi neema wananchi wa Mtwara kutokana na uchimbaji wa gesi na kwamba kabla ya kufikiria kuisafirisha kwenda Dar es Salaam ni muhimu ahadi hiyo ikatekelezwa.
 

“Zaidi ya miaka 21, Barabara ya Mtwara - Dar es Salaam haijaisha, mikoa mingine zinajengwa barabara zenye kilomita nyingi na zinakamilika na kuiacha hii ya kusini… hata juzi nimepita hapo bado barabara ni ya vumbi,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Mtwara, Sheikh Marijani Dadi alishauri pande mbili zinazopingana kukutana ili kufikia uamuzi.
 

Waziri amshukia Mbunge
Wakati viongozi hao wa dini wakitoa misimamo yao, jana Profesa Muhongo alimjia juu Murji kwa kuunga mkono msimamo wa wananchi kupinga usafirishwaji wa gesi hiyo.
“Hatukubaliani na Murji hata kidogo, hayo ni maoni yake yeye mwenyewe na mtazamo wake. Tusikubali kuvunjavunja mikoa yetu kwa kisingizio cha rasilimali zilizopo katika wilaya zetu,” alisema na kuongeza:

“Kabla ya kuanza mradi huo, Serikali iliwashirikisha wananchi wakiwamo wabunge wote wa mikoa ya Mtwara na Lindi ambao walihudhuria vikao mbalimbali, kulipwa posho na kukubaliana kwa pamoja mikakati iliyowekwa na Serikali.”
Alisema utafutaji wa mafuta na gesi bado unaendelea katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi, Morogoro, Tabora na katika kina kirefu cha maji kuanzia katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji mpaka Kenya.
“Hatutegemei gesi hiyo ikipatikana wananchi wa mikoa husika nao waandamane kutaka kuhodhi rasilimali za gesi asilia,” alisema.
 

Akijibu hoja ya Waziri Muhongo jana Murji alisema: “Mimi ni mmoja wa wabunge walioshiriki vikao hivyo na kulipwa posho, lakini posho ile ilikuwa stahiki yangu kama ambavyo Muhongo alilipwa pia. Ila sasa napinga kwa sababu haya yanayofanyika, siyo tuliyokubaliana kwenye vikao hivyo.” Hata hivyo hakufafanua.
 

Bomba la gesi Dar
Profesa Muhongo alisema uamuzi ya kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam una manufaa makubwa kwa kuwa Dar es Salaam kuna mitambo mingi ya kufua umeme na pia jiji hilo linachangia karibu asilimia 80 ya mapato ya nchi pia itatumika viwandani, katika magari na majumbani.

“Tunajenga bomba hili kwa sababu za kiuchumi, tuna viwanda 34 vinavyotumia gesi asilia kuzalisha bidhaa. Mfano, kampuni moja ya kufua umeme kwa kutumia mafuta inatumia Dola1.7 milioni (za Marekani) kwa siku, ndiyo maana tumekubaliana baada ya miezi 18 tutaachana na uzalishaji wa umeme huu wa mafuta,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza:
“Umeme unaozalishwa kwa mafuta uniti moja, tunalipia senti 30 hadi 45 ya Dola za Marekani, lakini tukianza kutumia umeme wa gesi tutakuwa tukilipia senti sita hadi nane ya dola.”

Alisema Serikali itaokoa trilioni1.6 kila mwaka utakapoanza kutumika umeme wa gesi asilia… “ Pia gesi ikitumika Jiji la Dar es Salaam katika viwanda na majumbani itaokoa kiasi cha Dola202 milioni za Marekani kwa mwaka.”
Alisema pia Serikali ina mpango wa kuzalisha umeme kwa wingi zaidi ili kwenda sambamba na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano (2010-2015), kwamba ifikapo mwaka 2015 taifa liwe na uwezo wa kuzalisha umeme usiopungua megawati 2,780.

“Lengo ni kutaka uchumi ukue kutoka asilimia sita ya sasa mpaka nane hadi 10, tunataka kuwa na umeme wa uhakika na siyo kutegemea mvua ambazo hunyesha kwa kudra za Mwenyezi Mungu,” alisema na kuongeza:
“Bomba hili tunalijenga kisasa zaidi kiasi kwamba hata likikamilika, tunaweza kutoa gesi katika njia mbalimbali kwa ajili ya wakazi wa Mtwara na Lindi, pia tunataka lisiishie Dar es Salaam tu, bali liende katika mikoa mingine ya Kaskazini, Mashariki na Magharibi.”
 

Alisema gesi hiyo kutoka Mtwara itawezesha mitambo mipya itakayojengwa Kinyerezi (Dar es Salaam), kufua umeme zaidi ya Megawati 990 na mwingine kiasi kisichopungua Megawati 520 utafuliwa Somanga Fungu (Lindi).
Suala la gesi kwenda Dar es Salaam limezua mjadala nchini hasa baada ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuandamana Desemba, 27 mwaka jana wakipinga uamuzi huo wa Serikali kabla ya juzi Murji na Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mikindani, Ali Chinkawene kuungana na wananchi na vyama vingine vya siasa kupinga mpango huo.
                           CHANZO CHA HABRI GAZETI LA MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate