Zaidi
ya watalii 19 wakiwemo waingereza na wafaransa ,wamefariki Kusini mwa
Misri baada ya puto la joto walimokuwa kulipuka katika mji wa Luxor.
Ripoti zinaarifu kuwa kulikuwa na watalii ishirini katika puto hilo.
Moto na mlipuko vilisikika kabla ya puto hilo kuanguka Magharibi mwa Luxor.
Duru zinasema kuwa takriban maiti wanane walipatikana katika eneo la tukio.
Mji wa Luxor uko kwenye ukingo wa mto Nile, makao ya kale ya pharao. Ni eneo lenye sifa tele kwa watalii
Mwakilishi
wa makamapuni manane ambayo yanatengeza putu hizo, katika eneo la Luxor
alisema kuwa mlipuko wa gesi ulitokea wakati puto hilo likiwa umbali wa
futi alfu moja kutoka ardhini.
''Kulikuwa
na abiria 20 kwenye puto wakati wa ajali hiyo. Mlipuko ulisikika na
abiria 19 wakafariki. Abiria mmoja na rubani wa puto hilo
walinusurika,'' alisema mwakilishi huyo, Ahmed Aboud.
Wizara
ya mambo ya nje ya Uingereza iliambia BBC kuwa inatafuta taarifa kutoka
kwa wenzao nchini Misri kuthibitisha taarifa za majeruhi waingereza.
No comments:
Post a Comment