REAL MADRID imefanikwa kuwang’oa Barcelona katika kombe la mfalme (Copa Del Rey) kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-1 ndani ya uwanja wa Nou Camp.
Shujaa na nyota wa mchezo alikuwa ni Cristiano Ronaldo aliyeifungia Real Madrid mabao wawili.
Real Madrid inasonga mbele kwa jumla ya magoli 4-2 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Santiago Bernabeu.
Bao la kwanza la Real Madrid lilifungwa na Ronaldo kwa njia ya penalti katika dakika ya 14.
Ronaldo aliingia na mpira ndani ya eneo la hatari la Barcelona, akakatwa na Gerard Piqué na mwamuzi hakusita kutoa penalti.
Dakika ya 51 kipa wa Real Madrid Diego Lopez alilazimika kuruka kama mkizi kuokoa shuti kali ya Sergio Busquets na kuwa kona isiyozaa.
Dakika ya 57 Ronaldo akaindikia Real Madrid goli la pili baada ya shambulizi la kushtukiza.
Sami
Khadira alipiga mpira mrefu uliomkuta Di Maria aliyewalamba chenga
mabeki wa Barcelona na kuachia mkwaju uliopanguliwa kwa mguu na kipa José Manuel Pinto.
Mpira ukamkuta Ronaldo aukweka kifuani na bila papara akaushusha mguuni na kuachia shuti dhaifu liliojaa wavuni.
Kuanzia hapo Barcelona walifunikwa na kuzimwa kabisa huku wakinyiwa nafasi ya kucheza mpira wao wa pasi fupi fupi.
Ukawadia wasaa wa Real Madrid kuandika bao la tatu.
Kona iliyopigwa na kiungo Ozil dakika ya 68 ikamkuta beki chipukizi Raphael Varane aliyeruka hewani na kuujaza mpira wavuni.
Dakika
ya 82 Ronaldo alipokea pasi ndefu ya Xabi Alonzo na kuingia nao ndani
ya kisanduku cha Barcelona na kuachia mkwaju uliopanguliwa na Pinto.
Hatimaye
Barcelona wakapata bao la kufutia machozi dakika ya 89 kupitia kwa beki
wa kushoto Jordi Alba kufuatia pasi ndefu ya Iniesta.
Katika
mchezo huo Barcelona ilipiga mashuti matatu yaliyolenga goli dhidi ya
manane ya Real Madrid, wakapata kona 7 huku Real Madrid wakiambulia kona
3.
Madrid sasa itavaana na Atletico Madrid au Sevilla katika hatua ya fainali.
No comments:
Post a Comment