Kwa mara nyingine matumaini ya klabu ya Arsenal, kumaliza ukame wa miaka
zaidi ya saba ya bila kunyakuwa kikombe chochote yamepotea mchana wa
leo,baada ya kupoteza mchezo wao wa marudiano dhidi ya klabu ya
iliyoshuka daraja msimu uliopita, Blackburn Rovers.

COLIN
KAZIM - RICHARDS mchezaji anayecheza kwa mkopo Blackburn Rovers
amefunga bao pekee lililoitupa Arsenal nje ya michuano ya kombe la FA.
Wakati
Arsenal ikiingiza wachezaji wake watatu kwa mpigo Theo Walcott, Santi
Carzola na Jack Wilshere dakika ya 70 ili kusaka ushindi, ikajikuta
inafungwa bao dakika ya 72 lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

Furaha ya goli
Kazim aliyeazimwa kutoka Galatasaray
ya Uturuki aliufumania mpira uliotemwa na kipa Szczesny na kuachia
shuti lilogonga nguzo ya kulia kabla ya kujaa wavuni
Dakika
15 za mwisho mpira uliweka kambi ya kudumu kwenye lango la Blackburn,
Arsenal waliokuwa nyumbani wakafanya mashambuli ya mfululizo lakini safu
ya ulinzi wageni ikongonzwa na kipa Jake Kean ilikuwa imara kufagia
kila hatari.
Heka heka uwanjani
Arsenal: Szczesny,
Coquelin, Vermaelen, Koscielny, Monreal, Diaby, Rosicky (Wilshere 70),
Arteta, Gervinho (Walcott 70), Oxlade-Chamberlain (Cazorla 70), Giroud.
Blackburn:
Kean, Orr, Dann, Grant Hanley, Martin Olsson, Pedersen, Williamson,
Lowe, Markus Olsson (Bentley 63), Kazim-Richards, Rhodes (Goodwillie 82) Via www.saluti5.com

No comments:
Post a Comment