Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa kijiji cha Kineng’ene kata ya Mtanda wilaya ya Lindi mjini kujiunga na huduma ya mfuko wa afya ya jamii (CHF) unaotolewa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ili waweze kuepukana na gharama za matibabu za mara kwa mara wanazolipa pindi wanapougua wakati ambao hawana fedha.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata ya
Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji
hicho leo, Feb 16, 2013.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Lindi Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho, Feb 16, 2013.
Mkazi
wa Kijiji cha Ng’apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya
matibabu ya Huduma ya Kadi ulkiopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa
mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kijiji hicho, Feb 16,
2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya kuzungumza wakati akihimiza
umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa matibabu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa kwenda kwenye
mkutano wa ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na
viongozi wa kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya
msingi ya kijiji cha Ng’apa, mkoani Lindi, Februari 16, 2013. Hatua
hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa dharura. Mama
Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa kufanyika
katika chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati
wa wananchi wa Kijiji cha Ng’apa wakimsiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilipowahutubia mkutano
wa hadhara jana, Feb 16, 2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na viongozi wa Tawi la Chama
Cha Mapinduzi la Nanyanje lililoko katika kata ya Chikonji katika wilaya
ya Lindi kwa ajili ya mkutano na viongozi wa Tawi na baadaye na
wananchi wa kata hiyo tarehe 15.2.2013.
(PICHA NA JOHN LUKUI WA MAELEZO)
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
anayewakilisha wilaya ya Lindi akiongea na viongozi wa Kata ya Chikonji
kwenye tawi la Nawanje tarehe 15.2.2013.
Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto waliobebwa na mamaya wakati wa mkutano wa hadhara huko Nawanje.
Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wana CCM na wananchi wa kata ya Chikonji huko wilayani Lindi tarehe 15.2.2013
Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Katika kijiji cha Chijonji.
Mama
Salma Kikwete akimsalimia mama Fatuma Mohammed ambaye pamoja na umri
wake kuwa mkubwa naye alijumuika katika mkutano wa hadhara.








No comments:
Post a Comment