MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama
Salma Kikwete anatarajia kukabidhi kontena la futi 40 lenye vifaa tiba
vya thamani ya Sh700 milioni katika hospitali sita nchini.
Vifaa hivyo vya tiba ya kuzuia vifo vya mama na mtoto vilipatikana kupitia uchangishaji fedha uliofanyika katika Jimbo la Arizona nchini Marekani.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Wama, Daudi Nassib alisema lengo la taasisi hiyo kugawa vifaa hivyo ni baada ya tathmini ya huduma ya mama na mtoto iliyofanywa katika hospitali hizo. Alisema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kuboresha maisha ya wanawake na wasichana kwenye masuala ya afya.
“Malengo ya Wama ni kusaidia kuboresha utoaji wa matumizi ya huduma bora ya afya kwa wanawake na watoto kwa jumla kupitia ugawaji vifaa kwenye hospitali zenye mahitaji makubwa,”alisema Nassib.
Nassib alivitaja vifaa vitakavyokabidhiwa katika hospitali hizo kuwa ni pamoja na Mashine ya X-Ray, Mitungi ya gesi ya Oxygen,Utra Sound, mitambo pamoja na vitanda katika vyumba vya uangalizi wa karibu(ICU),
Alisema hospitali itakayokabidhiwa vifaa hivyo ni
pamoja na Hospitali ya Lugulai,Mtwara ,kitete,Tabora, Simiyu na Tumbi ya
mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment