KIUNGO
Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, jana ameiwezesha timu yake
kutimiza jumla ya Pointi 42, baada ya kuifungia bao pekee dhidi ya
Kagera Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Unaweza
kusema chochote juu ya kiungo huyu wa kimataifa mzaliwa wa Rwanda,
lakini ukweli utabaki pale pale kuwa kwasasa Niyonzima ndio roho ya
Yanga. Ni aina ya mchezaji ambaye utampenda tu bila kujali itikadi yako.
Niyonzima
aliipatia timu yake bao hilo katika dakika ya 65, baada ya kupokea pasi
nzuri kutoka kwa Oscar Joshua, ambapo alimpunguza kiungo wa Kagera,
George Kavila na kuachia shuti kali lililotinga katika engo ya nyuzi 90
na kumshinda kipa Hannington Kalyesubula, aliyebaki akiutazama tu mpira
huo wakati ukitinga wavuni.
Kwa
mara nyingine tena, Niyonzima aliwafundisha wachezaji wa Yanga namna ya
kutumia nafasi zinazojitokeza kama alivyofanya katika mechi iliyopita
dhidi ya Azam.
Washambuliaji
wa Yanga walishindwa kutengeneza mazingira ya kutumbukiza mpira wavuni
ikiwemo penalti walizozawadiwa mwishoni mwa kipindi cha kwanza na
kupotezwa na Didier Kavumbagu.
Kiuongo
Dumayo naye alionyesha uwezo wa kuachia mashuti ya nmbali ambapo shuti
lake moja liligonga mwamba huku linguine likipanguliwa na kipa.
No comments:
Post a Comment