Dar es Salaam.
Wakati Wakristo nchini wakijiandaa kuungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, bei ya vyakula jijini imezidi kupanda kutokana na sababu mbalimbali.
Wakati Wakristo nchini wakijiandaa kuungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, bei ya vyakula jijini imezidi kupanda kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza sababu ya kupanda kwa bei hizo mfanyabiashara wa Soko la Kisutu, Japheti Kibiriti alisema moja ya sababu ni baadhi ya magari yanayosafirisha bidhaa kukwama njiani kitokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Alisema bidhaa zilizopanda kwenye masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam ni mchele, nyanya, viazi karoti na unga wa sembe.
Kibiriti alisema bei ya nyanya imepanda ambapo tenga la ndoo mbili za plastiki sasa linauzwa kwa Sh50,000 kutoka Sh30,000.
Mchele unauzwa Sh2,400 hadi Sh2,600, karoti Sh2,000, viazi vinauzwa kwa Sh2,000, unga wa sembe kilo moja huuzwa Sh1700 huku pilipili hoho zikiuzwa kwa kilo moja Sh3,000.
Mfanyabiashara wa Soko la Buguruni, Bakari Mponda
alisema mkungu mmoja wa ndizi huuzwa kuanzia Sh22,000 hadi Sh30,000
awali mkungu huo ulikuwa unauzwa kwa Sh15,000.
Mponda alisema bidhaa zingine zilizopanda ni matunda mbalimbali na hiyo inasababishwa na magari kukwama njiani hivyo bidhaa nyingi kuharibika.
Kwa upande wa nguo, Debora Sanze ambaye alikuwa akinunua nguo za watoto katika eneo la Kariakoo alisema bei aliyoikuta haikuwa mbaya sana.
“Sioni tofauti ya bei na nilivyozoea kununua sikukuu zilizopita, labda kwa sababu nimezoea kununua duka moja,” alisema Sanze.
No comments:
Post a Comment