KAMA
iliyoripotiwa hapo awali kuwa warembo watakaoshiriki kinyang’anyiro cha
kumtafuta Miss Tabata 2013, watatambulishwa siku ya sikukuu Pasaka
katika ukumbi wa Dar Wes Park - Tabata, tayari wadhamini kadhaa
wamejitokeza kudhamini onyesho hilo.
Kwa
mujibu wa mratibu wa onyesho hilo, Godfrey Kalinga, wadhamini
waliojitokeza utambulisho wa Miss Tabata 2013 ulioandaliwa na Bob
Entertainment na Keen Arts, ni Konyagi, CXC Africa, Fredito
Entertainment, Saluti5 na Kitwe General Traders.
Kalinga akasema kwa uoande wa burudani, ni kama walivyosema mwanzoni itakuwa ni Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”.
Amesema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya fainali itakayofanyika Mei.
Mratibu huyo aliongeza kuwa warembo 25 wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala 2012.
No comments:
Post a Comment