ABDULRAHMAN SHERIFF, MOMBASA
WATANZANIA wanaofanya biashara mjini hapa wameeleza masikitiko yao kwa wanasoka wanaochezea timu ya Bandari kutoitwa timu ya taifa ya nchi yao, Taifa Stars.

Mohamed Mbwana kutoka Tanga alisema kwamba anashangaa ni kwa nini
wanaochagua wachezaji wa timu ya taifa hawafiki Mombasa kuwashuhudia
wanasoka wanaoichezea Bandari kutoka Bongo.
Mbwana aliliambia Mwanaspoti mara baada ya Bandari kuishinda Sony Sugar mabao 3-0 kwamba beki Meshack Abel na viraka David Naftali na Thomas Maurice wote wanacheza vizuri na wanastahili kuitwa Taifa Stars.
"Dar es Salaam na Mombasa ni karibu, benchi la ufundi lifike kuwashuhudia hawa wachezaji wanavyocheza kwa masilahi ya timu ya Taifa," alisema Mbwana.
Raphael Kamaliza wa Dar es Salaam alisema kwamba Abel ni beki mwenye kucheza kwa maarifa, Mohammed Banka anafanya vizuri katika nafasi ya kiungo wakati Naftali na Maurice wanastahili kuitwa kambi ya Stars.
Mbali na wachezaji hao pia Ivo Mapunda anayechezea Gor Mahia anafanya vizuri kwenye kikosi chake ingawa kocha Kim Poulsen amekuwa akisisitiza kuwa anawafuatilia.
Wachezaji hao wanne Watanzania wanaocheza Bandari waliisaidia kwa kiwango kikubwa timu hiyo iliyoteremshwa daraja mwaka 2011, kurudi Ligi Kuu msimu huu.
Mapunda pia alikuwa kipa wa Bandari lakini ilipoteremshwa daraja alijiunga na Gor Mahia na kuwa kivutio.

No comments:
Post a Comment