MPAMBANAJI, mfanyabishara na kiongozi mwenye
ushawishi mkubwa ndani ya Yanga hususani kwenye usajili, Seif Ahmed
'Seif Magari' amesisitiza kuwa kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima
ameshasaini Yanga na kama Simba na Malkia wao wa Nyuki walikuwa na
mipango naye wamechemka.
Haruna mwenyewe ambaye yupo jijini Dar es Salaam amekataa kukiri kama amesaini Yanga na ameendelea kusisitiza kuwa itajulikana msimu ukimalizika Mei 18 kwani atakuwa ameshaamua.
Seif, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Udhamini la Yanga, amekuwa akifanya usajili wa Yanga kwa kushirikiana na Abdallah Bin Kleb na benchi la ufundi kwa takribani misimu mitatu mfululizo sasa.
Kiongozi huyo amewahakikisha mashabiki wa Yanga kuwa wasiwe na wasiwasi wala wasitishwe na maneno ya Simba au Azam kwavile tayari amemsainisha Niyonzima mkataba wa miaka miwili muda mfupi kabla ya kwenda kwao wikiendi iliyopita kucheza mechi ya taifa lake la Rwanda dhidi ya Mali. Mali ilishinda 2-1.
Lakini, Haruna wikiendi hiyo hiyo alizungumza na Mwanaspoti jijini Kigali baada ya mechi na Mali, akatamka kwamba hajasaini Yanga kwavile anasubiri msimu umalizike na wakala wake aliyeko Ulaya anamtafutia timu na kwamba endapo mambo hayataenda sawa atasaini mkataba mfupi na klabu moja kubwa ya Tanzania.
"Niyonzima ni mchezaji halali wa Yanga baada ya kusaini mkataba wa
miaka miwili, hivyo utata kama ataondoka Yanga baada ya msimu haupo
tena, tupo makini na hatuwezi kumuachia mchezaji makini kama yule aende
Simba au Azam au timu nyingine ya hapa,"alisisitiza Seif licha ya kwamba
hakuweka bayana dau walilompa kwa madai kwamba ni siri ya mkataba na si
lazima jamii ijue.Haruna mwenyewe ambaye yupo jijini Dar es Salaam amekataa kukiri kama amesaini Yanga na ameendelea kusisitiza kuwa itajulikana msimu ukimalizika Mei 18 kwani atakuwa ameshaamua.
Seif, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Udhamini la Yanga, amekuwa akifanya usajili wa Yanga kwa kushirikiana na Abdallah Bin Kleb na benchi la ufundi kwa takribani misimu mitatu mfululizo sasa.
Kiongozi huyo amewahakikisha mashabiki wa Yanga kuwa wasiwe na wasiwasi wala wasitishwe na maneno ya Simba au Azam kwavile tayari amemsainisha Niyonzima mkataba wa miaka miwili muda mfupi kabla ya kwenda kwao wikiendi iliyopita kucheza mechi ya taifa lake la Rwanda dhidi ya Mali. Mali ilishinda 2-1.
Lakini, Haruna wikiendi hiyo hiyo alizungumza na Mwanaspoti jijini Kigali baada ya mechi na Mali, akatamka kwamba hajasaini Yanga kwavile anasubiri msimu umalizike na wakala wake aliyeko Ulaya anamtafutia timu na kwamba endapo mambo hayataenda sawa atasaini mkataba mfupi na klabu moja kubwa ya Tanzania.
Mkataba ni siri kati ya timu na mchezaji, sitaweza kusema tumempa kiasi gani na atalipwa mshahara wa shilingi ngapi, haya ni mambo binafsi ambayo yapo katika sehemu yoyote, ninachokwambia ni kwamba suala la Niyonzima limekwisha,"alizidi kusisitiza na kudai anashangaa wanaokuza ishu hiyo bila kuchunguza.
Alisema kuwa pamoja na Yanga kuwa na mikakati ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, mipango yao mikubwa ni kuingia na kikosi imara kwenye msimu ujao wa michuano ya kimataifa na kutwaa tena Kombe la Kagame.
Kwa mipango hii, huwezi kuruhusu mchezaji kama Niyonzima kuondoka Yanga, labda kwa uongozi mwingine, lakini huu wa sasa, tumejipanga kwa kila kitu kwenda kwa mujibu wa mikakati yetu, kwa kifupi hakuna cha kutusimamisha, alisema.
Niyonzima alipotafutwa na Mwanaspoti jana Ijumaa aligoma kuzungumzia suala la mkataba huo na Yanga kwa kusema kuwa anasubiri mara baada ya kumalizika kwa ligi.
Lengo langu kubwa ni Yanga kutwaa ubingwa na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, kama mchezaji nina kila ya sababu ya kuhakikisha lengo hilo linafikiwa, nina mkataba na Yanga, lakini hayo mambo mengine siwezi kuzungumzia kwa sasa,alisema Niyonzima.
Alisema anaheshimu mkataba wake na Yanga na kama viongozi wametoa ufafanuzi wa suala hilo, yeye hana cha kusema zaidi ya kusubiri ligi kumalizika na kuweka wazi kila kitu.
Ligi imebakia kidogo tu kumalizika, naomba muwe na subira kwani kwa sasa siwezi kusema chochote kuhusiana na Yanga zaidi ya kucheza mpira na kuiwezesha timu kushinda taji, baadaye ukweli utajulikana tu, alisema mchezaji huyo na kukwepa kuzungumzia kauli ya Seif.
Kiungo huyo pia alisema hatocheza mechi ya leo Jumamosi dhidi ya Polisi Morogoro mjini Morogoro kutokana na kutokuwepo katika mazoezi tangu aruhusiwe kwenda kuichezea timu ya Taifa. Nilitoa taarifa na nikaruhusiwa, hakuna sababu nyingine ya mimi kutocheza mechi hiyo zaidi ya kutofanya mazoezi na ninaweza kucheza chini ya kiwango endapo nitapangwa, inaniuma sana kuikosa mechi hiyo,alisema.
Bin Kleb amekuwa karibu na mchezaji huyo ambapo amekuwa akisisitiza kwa jeuri kwamba hakuna klabu yoyote ya Tanzania inaweza kumnunua jambo ambalo linaonyesha tayari walikuwa na makubaliano.
No comments:
Post a Comment