Mabingwa wa Ligi Kuu Bara mwaka 1999, Mtibwa Sugar jana
walilazimika walisubiri mpaka giza kuingia kufunga bao pekee la ushindi
katika mchezo wa ligi dhidi ya Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.

Ushindi huo, umifanya Mtibwa Sugar sasa kufikisha pointi 31 sawa na Simba na Coastal Union zinazoshika nafasi ya tatu na nne, huku wapinzani wao Mgambo wakibaki nafasi ya nane ikiwa na pointi 24.
Kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha mchezo kati ya maafande watupu, Prisons ya Mbeya na JKT Oljoro uliingia dosari mwishoni baada ngumi kuzuka.
Vurugu hizo zilianza baada ya askari mmoja wa Magereza kwenda jukwaa waliloketi mashabiki wa timu ya Oljoro na ndipo ngumi zilipoanza na kuwajumuisha hata wachezaji.
Ukiachilia mbali sakata hilo, mechi ya maafande hao ulikuwa na ushindani mkubwa, shukrani kwa bao pekee kwenye mchezo huo kutoka kwa Swalehe Idd lililoipa ushindi wa bao 1-0 Oljoro dhidi ya Prisons.
Imeandikwa na Moses Mashalla (Arusha) na Yakub Burhan (Tanga).
No comments:
Post a Comment