MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha,
Christopher Julius (18), amekamatwa na vipande 13 vya meno ya tembo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Suleimani Kova, alisema mwanafunzi huyo alikamatwa Machi 22,
mwaka huu eneo la Kimara Wilayani Kinondoni.
Alisema mwanafunzi huyo alikamatwa baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo walifika eneo husika na kufanikiwa kumkamata pamoja na vipande 13 vya meno ya tembo.
Alisema thamani ya vipande hivyo bado haijafahamika na wanaendelea na upelelezi kubaini kama mtuhumiwa huyo alikuwa peke yake au alikuwa na wenzake.
Katika tukio jingine, alisema wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wakiwa na bunduki mbili aina ya Short gun yenye namba za usajili AB44736 na ya pili ni Greener yenye namba za usajili 10883 pamoja na risasi 17.
“Mafanikio
ya kuwakamata wahalifu hao yalipatikana Machi 20, mwaka huu baada ya
polisi kupokea taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba eneo la Magomeni kuna
gari dogo linalotumika kama teksi lina majambazi.Alisema mwanafunzi huyo alikamatwa baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo walifika eneo husika na kufanikiwa kumkamata pamoja na vipande 13 vya meno ya tembo.
Alisema thamani ya vipande hivyo bado haijafahamika na wanaendelea na upelelezi kubaini kama mtuhumiwa huyo alikuwa peke yake au alikuwa na wenzake.
Katika tukio jingine, alisema wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wakiwa na bunduki mbili aina ya Short gun yenye namba za usajili AB44736 na ya pili ni Greener yenye namba za usajili 10883 pamoja na risasi 17.
“Tulifuatilia na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao walikuwa katika gari hilo na walikiri kuwa wanajiandaa kwenda kupora eneo la Kurasini ambapo wangepora kiasi cha shilingi milioni 80 katika ofisi za Wachina,” alisema Kova.
No comments:
Post a Comment