Tanga. Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga, limefikishwa
mahakamani kwa tuhuma za kutokulipa michango ya wafanyakazi 25 wa Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Pia, linadaiwa kulipa hundi hewa ya Sh4,434,716.06
Pia, linadaiwa kulipa hundi hewa ya Sh4,434,716.06
Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa
NSSF, Samson Maira mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga, Ramla Shehangilo
kuwa kanisa hilo halikuwasilisha michango ya watumishi wake kuanzia
Januari 2006 hadi Juni 2012, ikiwa na thamani ya Sh35,950,573.63.
Aliendelea kudai kuwa, kati ya 35,950,5673.63 ni deni halisi la michango ya wafanyakazi wa kanisa hilo, ambao ni wanachama wa NSSF ambalo baada ya makubaliano lilitakiwa kulipwa kwa awamu hadi Aprili 2008.
Pia, Maira alidai katika kipindi hicho, Kanisa hilo lilitoa hundi ya Sh4,434,716.06, ikiwa ni malipo ya wanachama wa NSSF, lakini ilipofikishwa benki ikabainika ni hewa.
Hata hivyo, hakuna mwakilishi yeyote wa kanisa hilo aliyehudhuria mahakamani na Hakimu Shehagilo alitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa kanisa hilo, kwa kukaidi wito wa mahakama.
No comments:
Post a Comment