Siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa
Katoliki duniani, Papa Francis amewashangaza wengi mengi kwa kukataa
kuvaa viatu vya kifahari na msimamo wake kuwekwa wazi kuwa hatavumilia
makasisi watakaotenda uovu.
Papa Francis 1
Tayari, Papa Francis ameelezwa kuwa kiongozi
asiyetaka makuu, mhafidhina na mtu ambaye hataweza kubadili mengi katika
kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.2 duniani.
Katika siku mbili za uongozi wake, Papa Francis
amelithibitisha hilo kwa kutokea hadharani akiwa amevaa viatu rahisi,
vyeusi na kuachana na vyekundu vya kifahari vilivyopendelewa na
mtangulizi wake, Benedict VXI.
Kutoka Uk 1
Katika uongozi wake, siku zote Papa Benedict, alivaa viatu vyekundu vilivyotengenezwa kwa mkono, jambo ambalo Papa Francis anaonekana kuachana nalo.
Watu walio karibu naye Papa Francis, wanaeleza
kuwa kabla ya kuondoka Buenos Aires, Argentina kwenda Rome, Kardinali
Jorge Mario Bergoglio, kama alivyojulikana awali, alivaa viatu rahisi
vya rangi nyeusi, na kuwafanya marafiki zake, wakiwamo mapadri kutaka
kumnunulia viatu vingine vipya.
“Siku ile aliyoondoka mjini Buenos Aires kuelekea Rome kwa ajili ya mkutano wa uchaguzi wa Papa (conclave), marafiki zake walimpa zawadi ya viatu. Yeye, siku zote amekuwa akitokea hadharani akiwa amevaa nguo rahisi, viatu vya kawaida,” walieleza mapadri hao kutoka Amerika Kusini walipozungumza na Kituo cha Redio Vatican.
Mbele ya makardinali 106
Juzi Ijumaa alipokutana na makardinali 106,
kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, licha ya kuonyesha uso wa furaha
na kuwatania aliwaonya makardinali hao kuhusu wajibu wao kama viongozi
wa kanisa maeneo mbalimbali duniani akiwataka kutosahau kuwa hawarudi
kwenye ujana.
Katika ukumbi wa Sala Clementina, ulioko Vatican Papa Francis pia aliwataka makardinali hao wakiwamo waliomchagua kuwategemea zaidi vijana aliosema ndio nguzo kuu muhimu ya ustawi wa Kanisa Katoliki, huku aliwashauri makardinali kusaka njia sahihi ya kueneza Ukristo pande zote za uso wa dunia katika karne ya 21.
Aidha, alimsifu mtangulizi wake, Papa Benedict kwa
uamuzi wa kijasiri wa kustaafu, akieleza kuwa ni uamuzi wa busara,
wenye kuonyesha ukomavu na kuwataka wasichoke kuiga matendo mema.
Yaliyomo kitabuni mwake
Msimamo kuhusu makasisi
Katika kitabu hicho, Papa Francis anazungumzia maisha ya utauwa (usafi wa moyo), uadilifu na maovu akiweka wazi msimamo wake usio wa mzaha na kuruhusu mijadala baina ya makundi ya imani tofauti, msimamo ambao unaweza kupingwa na baadhi ya Wakatoliki wenye msimamo mkali.Kwa maneno yake, Papa Francis anaonyesha kuwa mtu mwenye akili, anayefikiri haraka, mjuzi wa mambo, anayechanganya uhafidhina wa kijamii na akiwa mwenye msimamo mkali wala kutokukubali upuuzi kwa mambo asiyoyapenda au kuyakubali.
Kiongozi huyo ameahidi kutumia Jumamosi ya Machi 23 kumtembelea mtangulizi wake, Papa Benedict katika jumba analoishi huko Castel Gandolf, kusini mwa Rome na anaeleza kuwa kanisa limepitia nyakati ngumu. “Kumekuwa na vipindi vingi, majaribu mengi. Kumekuwa na vipindi vigumu, lakini, kanisa limesimama imara.”
“Ni dhahiri kuwa katika historia yake, kanisa limebadilika mno, sioni sababu za kwa nini tusikubali mabadiliko na kuwa utamaduni wetu wa sasa,” anaeleza.
Kupitia kitabu, On Earth and Heaven (Duniani na Mbinguni)
alichokiandika akiwa kardinali, Papa Francis alitoa taswira yake kama
mtu mwenye dhamira safi hasa katika masuala ya kusaidia jamii, muumini
thabiti anayeamini katika majadiliano baina ya makundi ya imani tofauti.
Msimamo kuhusu makasisi
Papa Francis ameonyesha wazi kuchukizwa na matendo
ya makasisi (mapadri) wasio waadilifu, ambao kwa miaka mingi
wamelifedhehesha kanisa na kwamba yeye hakubaliani na wanaoficha maovu
ya baadhi ya mapadri ukiwamo ulawiti.
“Suala la useja (mapadri kutokuoa) kwamba ndicho
chanzo cha ulawiti linaweza kusahaulika,” anaeleza katika kitabu hicho.
“Endapo padri ni mlawiti, alikuwa hivyo hata kabla ya ukasisi wake.
Lakini, hili linapotokea, lisiangaliwe kwa mtazamo tofauti, lisifichwe.
Kama kiongozi, hutakiwi kutumia madaraka yako kuangamiza maisha ya mwingine.”
Kama kiongozi, hutakiwi kutumia madaraka yako kuangamiza maisha ya mwingine.”
Kuhusu hatua gani atachukua, wakati akiwa
Kardinali Bergoglio, alijibu kuwa hawezi kukubaliana na waovu, lakini
alipoulizwa kama askofu angechukua hatua gani dhidi ya mapadri wa aina
hiyo, alijibu,” Nitamfukuza kazi, kisha kumshtaki, jukumu langu ni
kuweka usafi wa kanisa mbele.
“Hili ni suluhisho kwa matukio kama hayo kama
jinsi ilivyopendekezwa Marekani; lakini si kuwahamisha wakosaji kutoka
parokia moja kwenda nyingine.
“Huu ni upuuzi, kwani hata huko wataendeleza tatizo hilo. Jibu sahihi kwa tatizo hili ni kutowavumilia.”
Katika kitabu hicho, Papa Francis anazungumzia maisha ya utauwa (usafi wa moyo), uadilifu na maovu akiweka wazi msimamo wake usio wa mzaha na kuruhusu mijadala baina ya makundi ya imani tofauti, msimamo ambao unaweza kupingwa na baadhi ya Wakatoliki wenye msimamo mkali.Kwa maneno yake, Papa Francis anaonyesha kuwa mtu mwenye akili, anayefikiri haraka, mjuzi wa mambo, anayechanganya uhafidhina wa kijamii na akiwa mwenye msimamo mkali wala kutokukubali upuuzi kwa mambo asiyoyapenda au kuyakubali.
Kiongozi huyo ameahidi kutumia Jumamosi ya Machi 23 kumtembelea mtangulizi wake, Papa Benedict katika jumba analoishi huko Castel Gandolf, kusini mwa Rome na anaeleza kuwa kanisa limepitia nyakati ngumu. “Kumekuwa na vipindi vingi, majaribu mengi. Kumekuwa na vipindi vigumu, lakini, kanisa limesimama imara.”
Hata hivyo, katika misa yake ya kwanza, Alhamisi,
Papa Francis alieleza kuwa kanisa hilo halina budi kwenda na wakati,
kukubali mabadiliko.
“Ni dhahiri kuwa katika historia yake, kanisa limebadilika mno, sioni sababu za kwa nini tusikubali mabadiliko na kuwa utamaduni wetu wa sasa,” anaeleza.
Alieleza kuwa mafundisho ya msimu ya Kikatoliki, msimamo kuhusu mashoga, ndoa za jinsia moja, hayawezi kubadilika.
Pia, anaeleza kuwa utoaji mimba ni tatizo la kisayansi zaidi, lakini ambalo haliwezi kukubaliwa na kanisa.
Kuhusu utandawazi, Papa Francis alieleza kwamba
hakubaliani nao kwa kuwa mfumo huo hauheshimu tamaduni. “Aina ya
utandawazi unaofanya vitu vyote kuwa sawa ni aina ya unyama,” anaeleza
akiongeza kwamba tofauti za kitamaduni hazina budi kudumishwa.
“Hatimaye, utandawazi unageuka njia ya kuwatumikisha wengine,” alisema.
No comments:
Post a Comment