LASTECK ALFRED
KITENDO cha Yanga wa kuendelea kung'ang'ania kileleni mwa msimamo wa ligi huku ikihesabu dakika tu kuivua ubingwa Simba, kimezidisha presha Msimbazi na Kocha Patrick Liewig amewachomoa mastaa kumi kikosini.
Liewig amezungumza na Mwanaspoti na kusisitiza kwamba hataki masihara kwenye kikosi hicho na kuanzia sasa atatoa nafasi kwa wachezaji wengi vijana ili kuongeza umakini na kurudisha morali ya timu kwavile katika mechi zilizopita wameonyesha wanaweza na ndio maana hata walishinda mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.

Ingawa Liewig hakuingia kiundani lakini Mwanaspoti linajua kwamba
amekaa kikao kirefu na uongozi baada ya mechi na Coastal Union na
kukubaliwa mpango wake wa kuwapiga chini wachezaji 10 wenye majina
makubwa ambapo hawatacheza mechi yoyote kuanzia sasa mpaka msimu
umalizike.
Hiyo ni katika kuhakikisha kwamba wanashinda mechi zote zilizosalia na kupata moja ya nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi kwani Yanga imezidi kupata kiburi na kuringia pointi 45 walizonazo. Azam ni ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 37 na Simba ni ya tatu kwa pointi 34.
Wachezaji hao 10 waliokumbwa na kisu hicho na hawatatumika kuanzia mechi ya Machi 27 dhidi ya Kagera Sugar ni Haruna Moshi Boban, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso, Amir Maftah, Abdallah Juma, Juma Kaseja, Felix Sunzu, Mrisho Ngassa, Komanbilli Keita na Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Kocha huyo aliwashauri Simba kwamba asilimia kubwa ya wachezaji hao
wameshuka viwango, hawajitumi na hawaisaidii timu kutokana na sababu
mbalimbali na uongozi ukamuunga mkono kwamba atumie vijana kwenye
michezo yote iliyosalia ukiwemo dhidi ya Yanga Mei 18.
Hiyo ni katika kuhakikisha kwamba wanashinda mechi zote zilizosalia na kupata moja ya nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi kwani Yanga imezidi kupata kiburi na kuringia pointi 45 walizonazo. Azam ni ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 37 na Simba ni ya tatu kwa pointi 34.
Wachezaji hao 10 waliokumbwa na kisu hicho na hawatatumika kuanzia mechi ya Machi 27 dhidi ya Kagera Sugar ni Haruna Moshi Boban, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso, Amir Maftah, Abdallah Juma, Juma Kaseja, Felix Sunzu, Mrisho Ngassa, Komanbilli Keita na Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba Liewig amewachambua wachezaji hao kwenye makundi tofauti kwamba kuna baadhi ni watovu wa nidhamu, wengine hawajitumi, baadhi wanatumia pombe na sigara kali, wapo wanaokesha klabu za usiku na hawataki kufuata utaratibu kambini na nje ya kambi.
Simba imekuwa ikisingizia kwamba baadhi ya wachezaji hao ni majeruhi na wengine kutoa sababu moja ya jumla ya utovu wa nidhamu bila kuingia kiundani.
Liewig mwenye misimamo mikali, amewaelezea viongozi huku akisapotiwa na Julio kwamba baadhi ya wachezaji hao pia hawana upendo baina yao na hata kuna wengine hawazungumzi kabisa iwe mazoezini au kwenye mechi jambo ambalo ni tatizo kubwa kama likiendekezwa kwavile wote wako kikosi cha kwanza na wanacheza nafasi ambazo zinategemeana kwa karibu hivyo ni rahisi mmoja kumhujumu mwenzie.
Kwa upande wa Kaseja imeelezwa kwamba amechoka hivyo ni wakati muafaka wa kumpa nafasi Abel Dhaira ambae amesajiliwa kwa fedha nyingi na amekuwa akisugua benchi.
Hatahivyo mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi alieleza kwamba kuna mabeki wawili wa kikosi cha kwanza hawana uhusiano mzuri na Kaseja na hawaongei.
Kocha pia alieleza kwenye kikao hicho kukerwa na kitendo cha Ngassa kuvua kitambaa cha unahodha na kukitupa chini wakati alipotolewa kwenye mechi dhidi ya Coastal Union na baadae mchezaji huyo akatamka wazi kwamba hajiskii raha kuendelea kuwemo Simba na hataongeza mkataba.
Kocha ameungwa mkono kwa asilimia kubwa na uongozi uliokuwepo kwenye kikao hicho ambao umekiri kwamba baadhi ya wachezaji hao wamechuja kwavile hawana muda wa kupumzika na kufanya mazoezi kwa wakati na vilevile wapo wanaodaiwa kushawishiwa na baadhi ya wanachama matajiri wacheze chini ya kiwango.
Simba inaondoka Dar es Salaam leo Jumamosi kuelekea Kagera lakini itasimama kwa siku tofauti kwenye mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora kucheza mechi za kirafiki.
CHANZO MWANASPOT
No comments:
Post a Comment