ZAIDI ya walimu 300 wilayani Mbozi wameweka rehani kadi za mashine za kutolea fedha benki (ATM).
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk Michael Kadege alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa kawaida wa mwaka wa Chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) cha walimu wilayani hapa kinachojumuisha pia wanachama kutoaka wilaya mpya ya Momba.
Dk Kadege alisema ni jambo la kusitikisha kwa walimu wanaoaminiwa na jamii kuwa waelevu kujiingiza katika mikopo ya namna hiyo inayowalazimu kutoa pia namba zao za siri na kuwaruhusu wakopeshaji kwenda kujichukulia fedha benki mara mishahara inapotoka.
“Walimu wametoa kadi wakakabidhi na namba zao za siri hivyo mkopeshaji anaamua mwenyewe akatoe shilingi ngapi kwenye akaunti husika. Sijui walimu hawa wakitapeliwa na mkopeshaji wa namna hii watamfikisha katika chombo
gani cha sheria kwakuwa hakuna mkataba wowote waliowekeana,” alisema Dk Kadege.
via Lukwangule blog

No comments:
Post a Comment