Daraja la Mto wa Jangwani Beach, Manispaa ya
Kinondoni, Jijini Dar es salaam liko hatarini kuvunjika kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha Jijini humo huku Wakazi wa eneo hilo wakieleza
kuwa pamoja na Serikali kuwa na taarifa imekuwa ikilifumbia macho tatizo
hilo.
Wakizungumza na Clouds Fm,
baadhi ya wakazi wa eneo hilo, wamesema kuharibika kwa daraja hilo
kumesababishwa na kitendo cha Wakandarasi wanaopewa zabuni ya kujenga
miundombinu ya barabara kutojenga katika kiwango kinachotakiwa.
Wakazi
hao wameongeza kuwa kutokana na ubovu wa miundombinu ya daraja hilo
wamekuwa wakipata adha kubwa kufuatia daraja kufunikwa na maji pindi
mvua zinaponyesha.
Wakizungumza
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jangwani Beach, iliyopo pembezoni mwa Mto
wa jangwani beach, ambao wanaeleza athari wanazokumbana nazo pindi mto
huo unapojaa maji ambayo huelekea moja kwa moja katika shule hiyo.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, EL– AJUAE MARO amesema
pamoja na kufikisha taarifa kwa serikali ya Mtaa wa Kilonga Wima na kwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam kuhusiana na
tatizo hilo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
No comments:
Post a Comment