Katika
kupunguza tatizo la Msongamano wa Magari jijini Dar es Salaam Serikali
kupitia Wizara ya ujenzi imetia saini ujenzi wa kivuko kipya cha kutoka
Dar es Salaam hadi Bagamoyo kitachokiwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya
watu 300 kwa wakati mmoja.
Akizungumza
wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko hicho
kitakachojengwa kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark Waziri wa Ujenzi
Dokta JOHN MAGUFULI amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho ni utekeleaji wa
ahadi zilizotolewa na Rais JAKAYA KIKWETE wakati wa kampeni za uchaguzi
za Mwaka 2010 sambamba na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi ya Mwaka 2005.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam SAID MECKY SADICK ameelezea namna
kivuko hicho kitakavyosaidia kupunguza tatizo la msongamano wa magari.
No comments:
Post a Comment