- WALIKODI NA KULALA CHUMBA NAMBA 208
- WALIINGIA USIKU WAKATOKA MCHANA KWEUPE
- AMA KWELI MAPENZI YA MASTAA NI MAJANGA
Na Mwandishi Wetu
Unaweza kukwepa matone ya mvua
lakini siyo kamera za Global Publishers Ltd, zinapoamua kukufanyia kazi,
ukibisha waulize Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mke wa mtu, Irene Uwoya.
Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za hali ya juu kuuficha ukweli
kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu, walinaswa na
kamera za Global kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo
Mbezi Beach, Dar es Salaam.
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda,
linathubutu kwa kuwa lina ushahidi wa kutosha kutamka kwamba Diamond na
Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, waliingia saa 8:24
usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.
Hili ni
skandali linaloweza kuweka rekodi ya kukaa kwenye vichwa vya watu kwa
muda mrefu ujao, kwani Uwoya siyo tu kwamba ni mke wa mtu, bali pia ni
juzijuzi tu alijidai amesahihisha makosa yake kisha akathibitisha
kurudiana na mume wake, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, baada ya kutengana kwa
kitambo kirefu kidogo.
Skendo hiyo, inakuja na picha yenye mshtuko
mkubwa kuhusu Diamond ‘Sukari ya Warembo’, kwani baada ya kumpitia
Uwoya, ni dhahiri kwamba ndani ya Klabu ya Bongo Movie amebakiza wa
kuhesabu, tena ni wale ambao mvuto wao ni wa kumulika kwa tochi,
vinginevyo, vinara wote ameshadondoka nao dhambini.
Chanzo cha habri ni Global Publishers.
Kwa kuanzia na
Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Aunt Ezekiel, Uwoya
ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unit pamoja na
warembo wengine kibao, ni wazi sasa mtandao wa ngono wa Diamond, unagusa
karibu asilimia 97 ya mastaa wote wa filamu na muziki nchini.
No comments:
Post a Comment