RAIS KIKWETE AWASILI NAIROBI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS WA NNE WA KENYA MHE UHURU KENYATTA.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara
baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
jijini Nairobi jana tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa
nne wa Kenya, Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake, Mhe. William
Ruto, katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo Aprili 9, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya
kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nne wa Kenya,
Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe. William Ruto katika
uwanja wa michezo wa Kasarani leo Aprili 9, 2013. Mama Salma Kikwete na
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batilda Burian wamesimama pembeni
na wenyeji wao.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa
heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais
wa nne wa Kenya, Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe.
William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo Aprili 9, 2013.(PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment