EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, April 2, 2013

Jamhuri ya Afrika ya Kati yapata serikali

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye ametangaza baraza jipya la mawaziri baada ya kufanyika mapinduzi, ambalo asilimia wanatoka kwenye kundi la waasi la Seleka na chama cha zamani cha upinzani.

Tiangaye, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu na kiongozi wa waasi, Michel Djotodia aliyeongoza mapinduzi na kujitangaza rais baada ya kuudhibiti mji mkuu wa Bangui, aliitangaza serikali hiyo mpya jana Jumapili jioni kupitia redio ya taifa. Mbali na kuwa rais, Djotodia amejiongezea nafasi ya waziri wa ulinzi.

Baraza hilo lenye mawaziri 34, linajumuisha tisa kutoka kundi la waasi wa Seleka, wanane wanatoka chama cha zamani cha upinzani na mmoja ni mshirika wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani, Francois Bozize, aliyelazimika kuikimbia nchi hiyo, baada ya waasi kuidhibiti Bangui. Mawaziri wengine 16 bado hawajulikani wanatoka makundi gani ya kiraia.
 
Nafasi muhimu zashikwa na Seleka
Nafasi za mawaziri wa petroli, usalama, maji na misitu, na mawasiliano, zimechukuliwa na waasi wa Seleka, ambapo wizara ya habari na mawasiliano ikiongozwa na Christophe Gazam Betty. Serikali hiyo mpya itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu, hadi hapo itakapoitisha uchaguzi mkuu ambao Bozize amepigwa marufuku kushiriki.
Rais aliyepinduliwa, Francois Bozize 
                                                  Rais aliyepinduliwa, Francois Bozize
Ijumaa iliyopita, Djotodia alitangaza kuongoza nchi kwa kuzingatia mkataba wa amani uliofikiwa mwezi Januari mwaka huu na ameahidi kuondoka madarakani mwaka 2016 na kwamba hatoshiriki katika uchaguzi.

Ufaransa na Marekani iliitaka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuheshimu mkataba wa kugawana madaraka uliosainiwa Gabon. Hata hivyo, Marekani imesema Waziri Mkuu, Nicolas Tiangaye, aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo kulingana na mkataba huo, ndiye kiongozi halali wa serikali.

Waasi wa Seleka walianza harakati za kuingia Bangui mwezi Desemba mwaka uliopita kabla ya kukubali kushiriki kwenye mazungumzo ya amani na serikali ya Rais Bozize. Baada ya siku kadhaa za kupora vitu na ghasia, wanajeshi waasi wameudhibiti mji wa Bangui kwa msaada wa kikosi cha Afrika katika ukanda huo.
 
Wanajeshi wengi waliouawa walikuwa watoto
Lakini taarifa za kushtua kuhusu watoto wanajeshi kuuawa katika mapambano ya kuudhibiti mji wa Bangui zimechapishwa na gazeti la Afrika Kusini jana Jumapili.
Mpiganaji mdogo wa Seleka 
                                                     Mpiganaji mdogo wa Seleka
Gazeti la Sunday Times limewanukuu wanajeshi wakisema kwamba wengi wa wanajeshi waasi waliouawa walikuwa ni watoto.

Afrika Kusini imekataa kulizungumzia suala hilo. Afrika Kusini ina wanajeshi wake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikiwa ni kikosi cha kudhibiti usalama nchini humo kabla ya kuanguka kwa Bozize, jitihada ambazo zimeshindwa. Wanajeshi wake 13 waliuawa katika mapigano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wiki iliyopita, Umoja wa Afrika uliusimamisha uanachama Jamhuri ya Afrika ya Kati na imewawekea vikwazo waasi wa Seleka, akiwemo Djotodia. Tangu ijipatie uhuru wake kutoka Ufaransa, mwaka 1960, Jamhuri ya Afrika ya Kati imeshuhudia mapinduzi ya mara kadhaa. Wasiwasi wa kidini umeongezeka katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya Wakristo, tangu Djotodia ambaye ni Muislamu kujitangazia urais.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate