MTOTO Ayoub Agen (6), mkazi wa kijiji cha Lusanje, kata ya
Mpombo, wilayani Rungwe, ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana
kisha kutoweka na kichwa chake.
Tukio hilo la kinyama linakuja siku chache baada ya baba mmoja wilayani humo kumzika mwanaye akiwa hai.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwan Athuman, tukio la kuchinjwa mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa chekechea lilitokea Machi 31, mwaka huu, saa 11:00 jioni, baada ya kuchukuliwa akiwa anacheza na wenzake.
Diwani alisema kufuatia tukio hilo, wananchi walimuua mtu mmoja ambaye hata hivyo jina lake halikufahamika mara moja kwa kumteketeza moto baada ya kumhisi kuwa ni miongoni mwa watatu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mtoto hayo.
Alisema licha ya jeshi hilo kuendelea na uchunguzi, hadi sasa hawajaweza kufanikiwa kupata kichwa cha marehemu na kwamba taarifa zinaonyesha tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina.
“Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye hajaweza kutambulika mara moja naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira ambapo mwili wake uliteketezwa kwa moto,” alisema kamanda.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo aliyeuawa ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 35.
Habari kutoka eneo la tukio zinadai kuwa wauaji hao wanadaiwa kuwa ni watu watatu baada ya mtuhumiwa kusulubiwa kabla ya kuawa, alikiri kuwa alikuwa na wenzake wawali ambao hata hivyo hakuwataja kwa majina.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Rafael Mwaikenda, akizungumza kwa simu alisema mtoto huyo alichukuliwa nyumbani kwao na watu watatu wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na muda mfupi baada ya taarifa kutolewa, wananchi walianza kumtafuta na kukuta mwili wake umetelekezwa kichakani huku ukiwa hauna kichwa.
Aliongeza kuwa wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigo mtuhumiwa huyo, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Wakati huohuo, watu watatu wamekufa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya katika matukio mawili tofauti ya ajili za barabarani mkoani hapa.
Katika tukio la kwanza lililotokea eneo la Mbalizi wilayani hapa, katika barabara ya Mbeya- Tunduma, watu wawili Meshaki Inkuru (24) na Saidi Ndasi (19) walikufa baada ya gari aina ya Toyota Chesser lenye nambari za usajili T 516 AAA lililokuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika kuwavamia wakiwa nje ya Hoteli ya Royal Tughimbe walikokuwa wakiendelea na sherehe za Pasaka.
Kamanda wa polisi aliwataja majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali Teuli ya Wilaya ya Mbeya ya Ifisi kuwa ni Shar Mkumbwa (20), Julieth Katemi (18) wote wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi.
Tukio lingine lililotokea eneo la Soweto ambapo mtu mmoja mtembea kwa miguu aliyetambuliwa kwa jina moja la Paul (60) alikufa papo hapo baada ya kugongwa na gari ambalo hata hivyo halikuweza kujulikana mara moja.CHANZO TANZANIA DAIMA

No comments:
Post a Comment