RAIS Jakaya Kikwete ameombwa kuingilia kati mgogoro wa wakazi
wa Kata ya Kurasini, Wilaya ya Temeke na Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ambayo inataka kuwahamisha kinyume cha sheria.
Akizungumza juzi, kiongozi wa wakazi
hao zaidi ya 2,000, Gustavu Mihanjo alisema wanashangazwa na uamuzi wa
wizara kudharau amri ya mahakama inayowataka kusimamisha bomoabomoa ya
nyumba za wakazi hao.
Alisema wataridhika endapo Rais Kikwete atafika katika eneo hilo ili
waweze kumueleza vitendo viovu wanavyofanyiwa na watendaji wake.
“Tunamuomba rais aje mwenyewe Kurasini na kutupa nasaha. Sisi wananchi tutaridhika kama atakuja yeye mwenyewe na sio kutuma ujumbe.
“Pia tunaomba hawa wanaovunja amri ya mahakama wachukuliwe hatua kali
kwa sababu sasa ni mara ya pili wanafanya kitendo hiki,” alisema
Mihanjo.
Alisema kuwa maelezo ya Waziri wa Ardhi kuwa eneo lote linatakiwa ili
kubadilishwa matumizi lilipaswa kutolewa siku 90 kabla ya kitendo
hicho kufanyika.
“Kurasini ni mahala petu pa makazi, bila ya ushauri wowote wanakuja
kutuletea amri ya kuvunja nyumba zetu wakati kesi bado ipo mahakamani,”
alisema.
No comments:
Post a Comment