Mahakama ya Kilele nchini Ghana hapo kesho Jumanne itaanza
kusikiliza kesi inayopinga ushindi wa Rais John Dramani Mahama kwenye
uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Disemba mwaka uliopita.
Kesi hiyo inadaiwa kuligawa taifa katika makundi mawili. Mpinzani wa
Mahama, Nana Akufo-Addo alikwenda mahakamani kupinga ushindi huo kwa
madai kwamba hila, udanganyifu na wizi wa kura vilitawala zoezi zima la
uchaguzi.
Weledi wa siasa za Ghana wanasema kesi hiyo ni changamoto kubwa kwa
demokrasia changa ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Mahakama hiyo ya
kilele inaweza kutoa hukumu ama ya kumuidhinisha Mahama kwa msingi
kwamba alichaguliwa kihalala au pia inaweza kuhukumu kwamba Nana
Akufo-Addo ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na vilevile inaweza ikaamuru
uchaguzi huo urudiwe upya.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, uchaguzi wa rais wa Disemba mwaka jana
ulifanyika kufuatia kifo cha rais John Atta Mills mwezi Julai mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment