Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Marekani itafuatilia kwa
makini hatua za viongozi wateule wa Kenya katika kukidhi matakwa ya
mahakama ya uhalifu ya kimataifa -ICC- kutokana na tuhuma
zinazowakabili.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari msemaji wa wizara hiyo Hilary
Renner amesema watashiriki ipasavyo katika kulifuatilia suala hilo.
Kutokana na kauli hiyo Sudi Mnette amezungumza na Geofrey Musila,
mwanasheria wa kimataifa na mchambuzi wa siasa za Kenya, aliyejikita
hasa katika masuala ya ICC na kwanza anaelezea kwanini marekani imeibuka
na suala hili wakati huu. Kuskiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika
za masikioni hapo chini.
No comments:
Post a Comment