MBUNGE wa Nkasi, Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya
kuuliza swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili
kujipatia fedha za kigeni.
Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy alisema kwa kuwa zao la
tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia nzima, lakini limendelea
kulimwa na kuchangia pato la mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania,
kwanini serikali isihalalishe kilimo cha bangi kama ilivyo kwa tumbaku
ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.
Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa pingamizi
dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa ni moja ya
mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri Malima alisema
kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la biashara na
linachangia pato la taifa.
“Hapa nchini bado bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini
kama utafiti utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la
kuingizia pato taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.
No comments:
Post a Comment