EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, April 5, 2013

Nauli mpya zapingwa kila kona.

SIKU moja baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kutangaza nauli mpya, wadau mbalimbali wa usafiri nchini wamepinga hatua hiyo wakisema ingeendana na vipato halisi vya Watanzania pamoja na huduma bora za vyombo husika.

Kaimu Mkurugenzi wa Sumatra, Ahmad Kilima alitangaza juzi kuwa ongezeko hilo limetokana na maombi ya wadau wa vyombo vya usafiri nchini, hivyo wameongeza kiwango kwa wastani wa asilimia 24.46 kwa daladala badala ya asilimia 149 zilizopendekezwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nicolaus Mgaya alisema suala hilo ni zito na litawaumiza wafanyakazi kwa kuwa litakuwa ni mzigo mkubwa kwao.

Alisema kwa sasa wafanyakazi hawaridhishwi na kima cha chini wanacholipwa, kwamba maisha yatakuwa juu na hivyo baadhi ya familia watoto watashindwa kwenda shule kabisa.

“Kupanda kwa nauli kutawaumiza watu wengi na wanafunzi wataumia zaidi, sidhani kama mzazi atakuwa na uwezo wa kumpa mwanafunzi nauli huku yeye mwenyewe akiwa anabanwa kwa mshahara mdogo anaolipwa,” alisema Mgaya.

Alidai kuwa serikali inaangalia zaidi mwekezaji kuliko kujali raia wake huku akitolea mfano wawekezaji wa mafuta na vyombo vya abiria bila kujali wananchi wanagandamizwa pia.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Julius Mtatiro alisema kupandisha nauli, serikali imewabebesha mzigo mkubwa wananchi tena bila kuangalia huduma ya vyombo vya usafiri.

Alisema kabla ya nauli kupanda serikali na wadau wa vyombo vya usafiri walitakiwa kuangalia kama huduma zao zimeboreshwa ndipo wapandishe nauli kulingana na mahitaji bora ya wananchi.

Mtatiro alifafanua kuwa hata kabla ya nauli kupanda watu walikuwa wanatembea kwa miguu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda daladala kwa sh 300 hadi 500.

“Hata wengine walishindwa kwenda kwao mikoani na hivyo hujichangisha na kwenda mara moja kila baada ya miaka mitano, sasa watashindwa kabisa kufanya hivyo,” alisema.

Alisema serikali ina mipango mibovu isiyozingatia maslahi na kipato kwa wananchi, na kuishauri kuliangalia suala hilo kwa mapana zaidi kabla ya utekelezaji wake kuanza.
Mmoja wa wananchi, Ruhazi Ruhinda alisema kuwa kiwango hicho kilichoongezeka kimewekwa kwa nia ya kuwaua wanyonge kwa vile hakiendani na hali halisi ya kipato cha Mtanzania wa hali ya chini.

“Mwananchi wa kipato cha chini mshahara wenyewe hautoshi, hivyo badala ya kufikiria kuongeza nauli hizo wangefikiria kuboresha miundombinu na huduma za usafiri kwanza,” alisema.
Aliongeza kuwa mamlaka husika zimekuwa hazitendi haki kwa wananchi, kwani awali umeme nao ulipandishwa bila kuzingatia uwezo wa vipato vya watu.
“Upandishwaji huu umefanywa kiholela, baada ya muda vyakula navyo havitakamatika kwa kisingizio cha nauli,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Hassan Mchanjama alisema wanapinga utaratibu wa Sumatra kupandisha nauli kwa asilimia 40 bila kujali kipato cha watu wa kawaida.
Akizungumza jana na gazeti hili alidai wameshtushwa na kitendo hicho ambacho kinadhihirisha wazi kuwa sekta nyingi za kijamii nchini zinashikiliwa na mafisadi wasiojali ugumu wa maisha.
Alisema wanapinga kupanda huko kutokana na utaratibu mbaya wa Sumatra wa kushindwa kuwasimamia wamiliki wa magari, madereva na makondakta katika uendeshaji wa huduma hiyo nchini.
Alitaja baadhi ya maeneo ambayo miaka yote yamekuwa yakilipa nauli tofauti na ile elekezi ya serikali kuwa ni Mbagala, Mbezi na Gongolamboto.
“Unajua hapa kuna ufisadi kwani katika kikao chetu cha Desemba mwaka jana, kati yetu, Sumatra na wamiliki wa magari tuliwapinga wasipandishe nauli hadi pale watakapoleta mchanganuo wao unaotuonesha kuwa wanapataje hasara katika uendeshaji,” alisema.
Alisema kuwa wamiliki walishindwa kutekeleza makubaliano hayo kitendo kinachodhihirisha wazi kuwa biashara hiyo inaendeshwa kihuni bila ya kutunza mahesabu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate