UTAFITI uliofanywa na Mradi wa Mfumo wa Kijamii wa Matibabu ya Virusi
vya Ukimwi (CoBaSys) unaonyesha maambukizi ya VVU yamezidi kuongezeka
hapa nchini na duniani kwa ujumla.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kiongozi wa mradi huo nchini Tanzania, Profesa Ernest Mallya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema ongezeko hilo limetokana na sababu mbalimbali.
“Kusudio la mkutano wa mwisho ni kuthibitisha ufanisi uliopatikana kutokana na ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali kitaifa na kikanda, ambao wanajishughulisha na kuzuia maambukizi na matibabu ya VVU na Ukimwi pamoja na matunzo ya waathirika katika ngazi za kimataifa na ngazi ya kikanda,” alisema Profesa Mallya.
Alisema mkutano huo utashirikisha matokeo ya utafiti uliofanywa na jopo la kitaifa kutoka nchi sita za Afrika, majadiliano kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa kuhusiana na sera na mikakati ya pamoja iliyoafikiwa na ukanda wa Kusini Mashariki mwa Afrika.
Alisema itasaidia
udumishaji wa mwitikio dhidi ya VVU na Ukimwi pamoja na mgogoro wa fedha
unaoendelea ulimwenguni ambapo wadau mbalimbali walioalikwa
watawasilisha matokeo ya ushirikiano uliokuwapo baina ya Afrika na Ulaya
katika kutathimini sababu mbalimbali zinazoathiri kuwapo au kutokuwapo
uzingatiaji wa matibabu na jinsi gani hali hiyo inaweza kupunguza
unyanyapaa na kutengwa kijamii miongoni mwa waathirika.Akizungumza Dar es Salaam jana, kiongozi wa mradi huo nchini Tanzania, Profesa Ernest Mallya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema ongezeko hilo limetokana na sababu mbalimbali.
“Kusudio la mkutano wa mwisho ni kuthibitisha ufanisi uliopatikana kutokana na ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali kitaifa na kikanda, ambao wanajishughulisha na kuzuia maambukizi na matibabu ya VVU na Ukimwi pamoja na matunzo ya waathirika katika ngazi za kimataifa na ngazi ya kikanda,” alisema Profesa Mallya.
Alisema mkutano huo utashirikisha matokeo ya utafiti uliofanywa na jopo la kitaifa kutoka nchi sita za Afrika, majadiliano kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa kuhusiana na sera na mikakati ya pamoja iliyoafikiwa na ukanda wa Kusini Mashariki mwa Afrika.
Naye, Mratibu wa Mradi wa CoBaSys, Giovanni Guaraldi, alisema washiriki katika mkutano huo pia watajadili tatizo la uendelevu wa matibabu ya VVU na Ukimwi pamoja na utegemezi kwa wafadhili.
“Mkutano wa mwisho wa CoBaSys unakusudia kujadili jinsi mifumo ya matibabu ya kijamii itakavyobiliana na changamoto mbalimbali za usoni mara nyingi, zikijumuisha mabadiliko ya VVU na Ukimwi kuwa magonjwa sugu, ukosefu wa fedha kutoka kwa wafadhili na ongezeko la ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma bora za afya,” alisema Guaraldi.
Alisema hata kama mifumo ya matibabu ya kijamii haitaweza kukabiliana vya kutosha na ongezeko la changamoto nyemelezi zinazoambatana na umri mkubwa wa watu wanaoishi na VVU, ongezeko la haki za kiraia na uraia utahakikisha haki za kiafya na za kijamii zinalindwa na kutakuwapo na upatikanaji wa huduma bora za afya kwa usawa katika ngazi za kitaifa na kimataifa.
Alisema mkutano huo ni sehemu ya mradi wa CoBaSys unaokusudia kuanzisha mtandao wa kikanda kwa ajili ya kuhakikisha sera ya afya inaziwezesha jamii kusaidia mipango ya utoaji wa dawa za kurefusha maisha ya waathirika (ARVs) kwa wagonjwa wenye VVU katika nchi za Kusini na Mashiriki mwa Afrika.
“Mifumo ya kijamii ya kuwatunza waathirika imekuwa ikisisitizwa na Serikali na asasi mbalimbali kwa sababu inahimiza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali, jamii ikihusishwa kikamilifu katika kubainisha matatizo na mahitaji yao, kisha kuchagua masuala yanayostahili kupewa kipaumbele na kuainisha rasilimali mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kukidhi mahitaji hayo,” alisema Guaraldi.
No comments:
Post a Comment