CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuingilia kati mgogoro wake na Serikali, ili kuilazimisha
itekeleze mapema matakwa ya walimu kabla hawajachukua hatua zaidi.
Kauli hiyo, imekuja kufuatia Serikali kudaiwa kupuuza hukumu ya mahakama pamoja na ushauri wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, iliyoelekeza pande zote mbili zikae kwa majadiliano zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema Serikali imeonyesha kutojifunza kutokana na mgomo wa walimu uliotikisa nchi nzima mwaka jana.
Alisema siku zote Serikali imekuwa haiwathamini walimu, licha ya kusema imekuwa ikiwajali siku zote.
Alisema
dharau ya Serikali, imeonekana wazi kwa sababu imeshindwa kuheshimu
vyama vya wafanyakazi, ambavyo vinatambuliwa kisheria.Kauli hiyo, imekuja kufuatia Serikali kudaiwa kupuuza hukumu ya mahakama pamoja na ushauri wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, iliyoelekeza pande zote mbili zikae kwa majadiliano zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema Serikali imeonyesha kutojifunza kutokana na mgomo wa walimu uliotikisa nchi nzima mwaka jana.
Alisema siku zote Serikali imekuwa haiwathamini walimu, licha ya kusema imekuwa ikiwajali siku zote.
“Kutokana na hali hii, tunatoa wito kwa walimu kuungana pamoja kuilazimisha Serikali kukubali kukaa meza moja na CWT kujadili mishahara ya walimu kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha.
“CWT kinatoa wito kwa Bunge kuingilia kati suala hili, ili kuepusha mgogoro unaoweza kujitokeza ikiwa Serikali itaamua kupanga mishahara ya walimu, bila kujadiliana na CWT.
“Tunatoa wito kwa wazazi wa wanafunzi kuingilia kati, kuna hatari wanafunzi milioni 10 kukosa masomo ikiwa walimu watagoma kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zao.”
Aprili 2, mwaka huu, makatibu wakuu wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi, ikiwamo CWT, walikutana na makatibu wakuu wa Wizara ya Utumishi wa Umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambapo Serikali ilieleza msimamo wake wa kutojadili mishahara kupitia majadiliano kwenye mabaraza ya kisekta, ikiwa ni pamoja na Baraza la Majadiliano la Walimu.
Kwa muda mrefu sasa, walimu wamekuwa wakiitaka Serikali iongeze mishahara kwa asilimia 100, posho za walimu wanaofundisha masomo ya sayansi asilimia 55, walimu wa sanaa asilimia 50 na posho ya mazingira magumu asilimia 30.
No comments:
Post a Comment