NEW YORK, MAREKANI
50 CENT ni mwanamuziki maarufu na tajiri duniani ambaye wengi wanadhani kwamba utajiri wake unatokana na kazi yake ya muziki.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, 50 Cent ametajwa kuwa katika nafasi ya tano akiwa na pato linalofikia Dola 124 milioni.
50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson, alizaliwa Julai 6, 1975. Muziki umempa umaarufu hadi kulifuta jina lake la kuzaliwa huku lile la 50 Cent likiwa juu.
Utajiri wake unahusishwa zaidi na dalili za
mafanikio zilizoanza kuonekana Februari 2003 baada ya kuibuka na albamu
yake ya kwanza ya ‘Get Rich or Die Tryin’ iliyofunika katika soko la
muziki nchini Marekani.
Katika siku nne za mwanzo, albamu hiyo iliuza nakala 872 na huo ukawa mwanzo mzuri wa kumtangaza 50 Cent katika ulimwengu wa muziki kwani jina lake lilipaa si Marekani tu bali hata kwingineko duniani.
Kwa 50 Cent, muziki ni sehemu tu ya utajiri kwani tayari, amejiingiza katika biashara mbalimbali zilizomfanya awe juu ikiwamo michezo ya kwenye video, vitabu, mavazi na nyinginezo.
Kama ambavyo amefanya msanii mwenzake, Dr. Dre, 50
Cent naye amejiingiza katika biashara ya ‘headphones’ ambazo zimekuwa
zikiuzwa kwa kutumia jina lake.
Mafanikio ya albamu ya ‘Get Rich or Die Tryin’ ni kama yalimpa 50 Cent jeuri ya kuutafuta utajiri.
Novemba 2003 baada ya albamu hiyo aliingia mkataba
wa miaka mitano na Kampuni ya Reebok kwa ajili ya mauzo ya bidhaa
zilizokwenda kwa lebo ya G-Unit. Bidhaa hizo ni pamoja na viatu na aina
mbalimbali za nguo.
Inadaiwa kwamba kwa mwaka 2006 pekee, 50 Cent aliingiza kiasi cha Dola 60 milioni zilizotokana na mauzo ya mavazi ya aina mbalimbali kupitia lebo ya G-Unit.
Sambamba na hilo, 50 Cent pia alisaini mkataba na
Kampuni ya Glaceau inayojihusisha na uuzaji wa maji yaliyokuwa na lebo
ya Formula 50. Mwaka 2007 Kampuni ya Coca-Cola iliinunua Glaceau kwa
Dola 4.1 bilioni. Ni katika kipindi hicho hicho Forbes walifanya
tathmini ya mauzo hayo na kukadiria kwamba 50 Cent alikuwa na mgawo
uliofikia Dola 100 milioni.
No comments:
Post a Comment