WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kutumia vema fursa
zenye tija zilizopo katika Akaunti ya Malkia ya Benki ya CRDB ili
kuharakisha harakati za maendeleo yao kibiashara na kijamii.
Hayo yalisemwa na Ofisa Masoko Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo
akiwasilisha mada katika kongamano la wanawake lililofanyika jijini Dar
es Salaam jana, likihusisha wajasiriamali wanawake.
Kiondo alisema kuwa harakati za maendeleo kwa mwanamke ni muhimu kwa
ustawi wa taifa na jamii na Malkia ya CRDB, ni njia sahihi
itakayomuwezesha mjasiriamali huyo kuokoa pato lake ambalo awali
lilikabiliwa na changamoto nyingi.
“Malkia Akaunti ni mkombozi wa kweli wa mjasiriamali mwanamke, ikibeba
tija nyingi na kumuepushia adha zilizopo katika aina nyingine ya
uwekezaji. Akaunti hii inatoa mkopo wa dharura wakati wa matatizo, wa
asilimia 80 ya akiba yako, bila kuathiri chochote,” alisema Kiondo.
Aliwakumbusha wanawake kuhakikisha wanaepuka kero na changamoto
zinazohatarisha harakati zao, kwa kuwekeza pesa zao kupitia akaunti
hiyo, ambayo imewanufaisha wengi miongoni mwa wanawake wenye malengo
tofauti.
Kongamano hilo la wanawake lilifanyika chini ya udhamini wa CRDB kupitia akaunti ya Malkia.
Wakizungumzia kongamano hilo, baadhi ya washiriki walipongeza mada na
ushuhuda uliotolewa na waelimishaji, ambao umewaongezea hamasa katika
kukabiliana na changamoto mbalimbali za kibiashara na kupanua wigo wa
maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment