Mtwara.
Hali ya usalama mkoani Mtwara ni tete. Mtu mmoja anaaminika kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na vurugu kubwa zilizozuka jana huko Mtwara baada ya kusomwa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati bungeni Dodoma jana.
Hali ya usalama mkoani Mtwara ni tete. Mtu mmoja anaaminika kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na vurugu kubwa zilizozuka jana huko Mtwara baada ya kusomwa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati bungeni Dodoma jana.
Aidha, askari wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamefariki dunia katika ajali wakitokea Nachingwea kwenda Mtwara ili kusaidia kutuliza vurugu hizo. Katika ajali hiyo, askari 20 walijeruhiwa, wengi wao vibaya na saba walinusurika.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula,
Dk Mohamed Kodi alithibitisha kupokea maiti moja na kuomba apewe muda
kutaja idadi ya majeruhi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa alidai kwamba hakuna mtu aliyefariki dunia wala majeruhi. Alisema watu 45 wamekamatwa.
Milio ya risasi za moto na mabomu ya machozi
vilisikika kila kona na hasa Mitaa ya Mdenga, Magomeni na Shengena Mjini
Mtwara ambako hali ilikuwa mbaya kutokana na kuwapo kwa mapambano kati
ya polisi na vijana.
Vurugu hizo zilitokana na hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kusisitiza kuwa bomba la gesi kutoka Mtwara na kuja Dar es Salaam litajengwa, jambo lingine linalodaiwa kusababisha ghasia hizo ni hatua ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja matangazo ya Bunge hivyo kuwakosesha wananchi fursa ya kusikiliza bajeti hiyo.
Akizungumzia kukosekana kwa matangazo hayo ya
televisheni, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alisema kukatika kwa
matangazo hayo kulitokana na tatizo la satelaiti katika mji huo na
Musoma.
Hata hivyo, wakazi wa Mtwara waliokuwa na ving’amuzi walipata fursa ya kuangalia matangazo hayo.
Pia vurugu hizo zilichangiwa na vipeperushi vilivyosambazwa na watu wasiojulikana wakitaka watu kuacha kufanya shughuli zozote na kukaa nyumbani ili kufahamu hatima ya mradi wa usafirishaji wa gesi kutoka Msimbati hadi Dar es Salaam kwa njia ya bomba.
Katika vurugu hizo zilizozagaa zaidi maeneo ya
Mikindani na Magomeni, wananchi pia waliharibu Daraja la Mikindani
linalounganisha Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.
Tangu asubuhi kama ilivyokuwa Mei, 17 mwaka huu,
Mji wa Mtwara ulikuwa kimya na huduma nyingi za kijamii zilisimama
ikiwamo usafiri wa pikipiki, daladala, mabasi maduka na masoko.
Ofisi ya Mtendaji Mtaa wa Msikitini, Kata ya Reli na Ofisi ya CCM Chikongola nazo zimeteketezwa kwa moto. Wanafunzi wa Shule za Msingi Shangani na Majengo walirejeshwa nyumbani baada ya mabomu ya machozi kurindima kuanzia asubuhi hadi mchana.
Vurugu
Katika Mtaa wa Magomeni, nyumba ya Mwandishi wa
TBC, Kassim Mikongolo iliteketezwa kabisa kwa moto na kundi hilo la
vijana. Pia nyumba za Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnein Murji na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa
Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia zilichomwa moto.
Mikongolo alisema nyumba yake ilichomwa moto saa
nne asubuhi... “Walipania kuchoma nyumba yangu kwa kuwa mke wangu ni
Koplo wa Jeshi la Polisi.”
Katika Mtaa wa Majengo, kundi la vijana lilivamia
Ofisi ya CCM Kata na Ofisi ya Serikali ya Kata na kuanza kuzibomoa. Pia
nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara-Mikindani, Ali Chinkawene
ilirushiwa mawe.
Ofisi ya Mtendaji Mtaa wa Msikitini, Kata ya Reli na Ofisi ya CCM Chikongola nazo zimeteketezwa kwa moto. Wanafunzi wa Shule za Msingi Shangani na Majengo walirejeshwa nyumbani baada ya mabomu ya machozi kurindima kuanzia asubuhi hadi mchana.
“Ni kweli Ofisi ya CCM na Ofisi ya Serikali ya
Kata zimebomolewa, nyumba yangu imerushiwa mawe,” alisema Chinkawene kwa
sauti ya chini na kukata simu.
Msimbati shwari
Wakati Mtwara Mjini hali ikiwa tete, katika Kijiji
cha Msimbati ambako gesi asilia inachimbwa, hali ni shwari na wananchi
walikuwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida.
“Maduka na soko vimefunguliwa, huku hali ikiwa
shwari kabisa ingawa msimamo wetu upo palpale, hatutaki gesi iende Dar
es Salaam kwa njia ya bomba,” alisema mkazi wa kijiji hicho, Juma Ayoub.
JWTZ wafariki ajalini
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa
Mtwara, Edward Gontako alithibitisha kutokea ajali hiyo ya askari wa
JWTZ, 41KJ Nachingwea na kusema wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Nachingwea.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Wilaya, Dk John Sijaona alithibitisha kupokea maiti za askari hao na kusema hali za majeruhi ni mbaya na kwamba mipango ilikuwa inafanywa kuwapeleka katika Hospitali ya Ndanda, Mtwara.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Wilaya, Dk John Sijaona alithibitisha kupokea maiti za askari hao na kusema hali za majeruhi ni mbaya na kwamba mipango ilikuwa inafanywa kuwapeleka katika Hospitali ya Ndanda, Mtwara.
No comments:
Post a Comment