Serikali imesema kuwa mpango wa ukaguzi wa ubora na viwango vya
bidhaa (PVOC) umesaidia kupunguza msongamano bandarini na kuwataka
wafanyabiashara nchini kuzingatia kuingiza bidhaa zenye ubora ili kuweza
kusaidia kuchochea uchumi wa nchi.
Akizungumza kwenye warsha iliyojumuisha wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo alisema wafanyabiashara wanapaswa kuwa makini katika masuala ya viwango kutokana na nchi nyingi kuwa makini katika masuala ya bidhaa zenye viwango. “Kuna haja ya kufanya jitihada ya kuboresha viwango ili kuweza kuongeza uzalishaji na uchumi wa nchi kwani tunapoongelea mambo ya viwango si kwa Tanzania tu bali ni pamoja na nchi zinazotuzunguka,” alisema Mapunjo.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Wakala wa
Kimataifa wa Ukaguzi wa Ubora wa Bidhaa nchini (BV), Jean –Michel
Marnoto alisema taifa lolote linalozalisha bidhaa kwa kuzingatia ubora
linajisafishia njia ya kufikia maendeleo kwa nyanja zote.Alisema lengo
la warsha hiyo ni kuungana na wateja na Watanzania kwa ujumla ili
kuelimishana na kubadilishana mawazo.dhi viwango na na ubora kulingana
na mahitaji ya soko.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS) Tumaini Mtitu alisema utaratibu wa uhakiki unasaidia kupunguza msongamano kutokana na shirika hilo kuwa na maabara chache za kupimia bidhaa.
Alisema kuna baadhi ya bidhaa zinazoingia nchini
zinashindwa kupimwa kutokana na kutokuwa na vipimo vya kupimia baadhi ya
bidhaa na kusababisha msongamano bandarini.
No comments:
Post a Comment