Na Imelda Mtem
MREMBO aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dustan ‘Jack’ amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro na kupata majeraha usoni na mguuni.
Akizungumza na Exclusive Star, Jack alisema Jumanne iliyopita walikuwa kwenye teksi yeye na marafiki zake wengine wakielekea maeneo ya Kihondo mkoani humo kumsalimia mjomba wake ndipo walipogongana na gari lingine katika ‘round about’ ya Msamvu na kumsababishia majeraha hayo.
Mara baada ya kupata ajali hiyo, Jack alisema alikimbizwa katika Hospitali ya Maria mkoani humo ambapo alipata huduma ya kwanza na sasa anaendelea vizuri.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri, angalau sasa naweza hata kutoka nje tofauti na mwanzo nilivyokuwa,” alisema Jack.

No comments:
Post a Comment