UNAPOKUWA mtu maarufu unafuatiliwa kwa vitu mbalimbali, pengine
unapokuja katika tasnia ya filamu ungependa kufahamu kuwa ni msanii gani
mwenye mvuto katika mitandao ya kijamii ambaye tu anpofanya tukio lake
na video hiyo ikawekwa katika mitandao ya kijamii na kufunguliwa na
kuangaliwa na watu wengi.
Kwa utafiti uliofanywa na FC msanii mwenye mvuto katika mitandao na
kufuatiliwa habari zake na watu wengi ni
Elizabeth Michal ‘Lulu’ ambaye
ndio msanii anayeongoza kwa video za matukio yake kuwa na mvuto na
kutembelewa na watu wengi baada ya video yake tu kuwekwa katika mtandao
kwa mujibu wa mtandao wa Youtube.
Kama ilivyo kwa wasanii wa nje ambao ujulikana kwa kuwa tofauti na
watu wengine ambao si nyota ndio maana
Ulimwengui sasa unamuongelea
msanii wa Marekani Lady Gaga kama ndio msanii mwenye marafiki wengi
katika akaunti yake ya facebook na kuwapita watu wote ambao ni wanachama
wa mtandao huo kwa nyumbani kipimo chetu ni kupitia mitandao pia.
Msanii Lulu ambaye ndio mwenye mvuto na wapenzi wengi katika mitandao
ya kijamii amewatupa wasanii wenzake ambao ndio nyota katika tasnia ya
filamu Swahiliwood katika mchakato huo Lulu kwa mwaka mmoja video zake
zilizowekwa kupitia youtube zimetazamwa na watu zaidi 749,961 idadi
ambayo haijafikiwa na msanii yoyote.
Katika kuonyesha kuwa msanii Lulu ni kipenzi cha watu ambao ufuatilia
habari kupitia mitandao mbalimbali hivi karibuni alipotoka lupango na
kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka ya utu uzima
yaani miaka kumi na nane video ya sherehe hiyo tayari imetazamwa na watu
58, 346 jambo ambalo linaonyesha kuwa ana mvuto kupitia mitandao.
.
.
Msanii mwingine ambaye pia video za mahojiano yake au matukio yake
nje ya filamu anayefuatia kwa mbali baada ya nyota Lulu ni Wema Abraham
Sepetu wengi hata mimi pia nilikuwa nafikiria anaweza kuwa na alama
nyingi kumpita Lulu lakini hali ipo tofauti kwani yeye video zake
zimetazamwa na watu 442,
874 kwa mwaka mmoja.
874 kwa mwaka mmoja.
Nyota mwingine wa filamu ambaye mahojiano yake yametazamwa na watu
wengi ni marehemu Steven Kanumba ambaye amejipatia alama nyuma ya msanii
ambaye alimtoa kisanaa Wema Sepetu marehemu ana alama 434, 104 naye kwa
takribani mwaka mmoja toka kuwekwa kwa Video zake kupitia mitandao ya
kijamii.
Baada ya kuingia mwanamume anayefuatia kuwa kivutio cha wapenzi wa
filamu kuangaliwa kazi zake kupitia mitandao ni mwanamke mlimbwende
Irene Uwoya ambaye video yake imeweza kutazamwa na watu 367, 707 kama
shindano tuseme anashika nafasi ya nne katika wasanii wanaovutia na
kufuatiliawa na wapenzi wa filamu Bongo.
Msanii anayefuatia naye kuvuta watu wengi kuangaliwa ni marehemu Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ huyu ameweza kutazamwa na watu wengi kupitia mitandao
kwa miezi saba tu baada ya video zake kuwekwa katika mitandao ya
kijamii na kupitiwa na watu 130, 754 katika wasanii wa filamu huyu ndio
anayefunga namba kwa wasanii wenye mvuto kupitia mitandao ya Video.
Hali inashangaza kwa wasanii ambao inaonekana kuwa ndio vinara wa
mauzo ya filamu lakini video zao zimetazamwa na watu wachache sana baada
ya kuwekwa na katika mitandao ya kijamii kwa kukosa watazamaji kwa
idadi kuwa ya watazamaji, jibu lake ni rahisi tu wasanii hawa
wameathiriwa kwa kukosa ukaribu na vyombo vya habari hasa Televisheni.
Wasanii waliothiwa na hali hiyo ni Ray ambaye kupitia mtandao wa you
tube yeye mahojiano yake yamepatika katika akaunti moja tu ya Youtube
Mkasi video yake imetazamwa na watu 59, 211 tu, na hakuna sehemu yoyote
ambayo ungeweza kupata mahojiano ya msanii huyo mwenye jina kubwa
Swahiliwood huku akiwa ni mwenye nafasi katika magazeti kuandikwa sana.
Wengine ni Jaqueline Wolper naye video yake inapatikana sehemu moja
tu na video yake kutazamwa na watu 50, 582 tu, Monalisa ambaye video
yake imetazamwa na watu 33, 500, akifuatiwa na Muhogo Mchungu mwenye
watu 30, 359, huku hali ikiwa mbaya sana kwa Aunt Ezekiel ambaye Video
yake zaidi miaka miwili imetazamwa na watu 23, 616 tu.
Wakati
wasanii wengine ni agharabu habari kupata habari kupitia mitandao ya
kijamii kama vile msanii mkubwa kama Jacob Stephen ‘JB’ msanii huyo hana
taarifa yoyote iliyopandishwa na kutazamwa na mtu, utafiti unaonyesha
kuwa msanii kama JB si mpenzi au hajui umuhimu wa kuongea na vyombo vya
habari jambo ambalo linamfanya kufanya mahojiano kwa njia ya simu tu na
watu kukosa takwimu kupitia mitandao ya kijamii.
Msanii ambaye baada ya mwaka mmoja inawezekana ndio akawa kinara wa habari zake kusomwa na kutazamwa na watu wengi ni King Majuto ambaye video yake ya mahojiano imewekwa kwa wiki mbili tu na kutazamwa na watu 31, 463 huku kazi zake alizoigiza zikiwa zimetazamwa watu zaidi 674, 461kwa baadhi ya komedi.
Huu ndio utofauti wetu sisi wa kawaida na nyota pia ikumbukwe kuwa
alama zilizotajwa ni Video zilizohusu mahojiano tu na si matangazo au
filamu za zilizowashirikisha wasanii hao, katika mchakato huo akinadada
ndio wameshika chati kwa kazi zao kuangaliwa katika mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment