MWIGIZAJI Mahiri wa filamu Swahiliwood Wema Abraham Sepetu ndiye msanii
anayelipwa fedha nyingi kuliko msanii yoyote wa filamu katika kushiriki
katika filamu kutoka kwa watayarishaji wengine ili uweze kumshirikisha
Wema Sepetu katika filamu yako kama mwigizaji bila kujali anacheza scene
ngapi gharama yake ni milioni kumi.
Wema ambaye kwa sasa anamiliki kampuni yake ya utengenezaji wa filamu Swahiliwood inayojuklikana kwa jina la Endless Fame Film anasema kuwa moja ya sababu inayomfanya aweze kuchaji gharama hiyo inajumuisha na kutumia kampuni yake pamoja yeye mwenyewe kuigiza katika filamu hiyo, kwa hiyo ni wajibu wa mhusika kumudu gharama hizo.
.

“Yaah
kama mtayarishaji ananihitaji kushiriki katika filamu yake atatakiwa
kunilipa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa kushiriki katika filamu
yake, lakini pia kuzingatia ratiba ya utendaji usiingiliane na kazi
zangu nyingine,”anasema nyota Wema.
Inasemekana kuwa Wema ndio msanii wa kike anayeuza filamu kuliko
mwigizaji wa filamu wa kike, pengine ndio sababu ya kuweza kutoza
gharama kubwa katika kushiriki filamu nje ya kampuni yake unapomuhitaji
Wema kwa ajili ya mapatano unaongea na mtendaji wake wa karibu Chiddy
Classic.
Gharama hizo ndio kubwa kwani hadi sasa msanii ambaye amelipwa kwa
kiwango cha juu ilikuwa ni milioni tano ikiwa kama ndio kikomo cha
malipo kwa wasanii wenye majina na wamiliki wa makapuni yao, msanii kama
Ray the Greatest hanunuliki kwani si rahisi kushiriki nje ya kampuni
yake ya RJ Company.
Irene, huwa nafurahia sana habari unazotuletea. Ila pia ujue kuwa tunatakiwa tujifunze na tuifundishe lugha yetu ya Kiswahili vizuri. Leo wanafunzi wamesoma hii habari halafu wameniuliza maana ya neno AGHARI. Nimeshindwa kuwajibu. Au ulimaanisha GHALI ambalo ndilo neno sahihi hapa?
ReplyDelete