UONGOZI wa Klabu ya Simba umekubali ombi la nyota wake Abdallah
Juma na Paulo Ngalema kutaka kuondoka katika klabu hiyo yenye maskani
yake mitaa ya Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Ngalema na Juma ni miungoni mwa wachezaji tisa wa Simba
waliosimamishwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patric Liewig kwa
madai ya utovu wa nidhamu kama ilivyo kwa Haruna Moshi ‘Boban.’
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia
Hanspope wameridhia matakwa ya nyota hao akisema wanawatakia mafanikio
katika malengo yao.
Hanspope alisema, msimu huu wanatarajia kufanya usajili mzuri ili
kuijenga timu na kuongeza kuwa wana mpango wa kuwatema nyota watano.
“Tunafanya usajili wa maana kuijenga timu, mpaka sasa tumeisasajili
nyota wanne, na tunawatema watano na katika hao hata wa Kimataifa wamo
maana kama Keita, amesha ondoka Simba,” alisema Hanspope.
Kuhusu kiungo wa timu hiyo Amri Kiemba kwenda Yanga, alisema hakuna
ukweli na wao wapo hatua za mwisho kumwongezea mkataba wa kuendelea
kucheza katika timu yao.
“Nimezungumza na Kiemba, sawa anawaniwa na Yanga…hana mpango kabisa wa
kwenda huko, lakini hata kama akitaka kwenda, sisi hatuwezi kumzuia,
tutakachofanya ni kuziba nafasi,” alisema na kuongeza:
“Na sio kama wenzetu wanavyojitamba, kuwa wanafanya usajili wa
kishindo, sisi hakuna usajili wa kishindo labda tukimsajili Ronado ndio
utakuwa usajili wa kishinde ila huu ni wa kawaida,”alisema.
Aliongeza kuwa, Simba bado inaendelea na zoezi la usajili na haiitaji kukurupuka ili waweze kupata nyota wazuri.
No comments:
Post a Comment