Wamiliki wa mabasi wanaowasaidia wapigadebe waendelee kufanya kazi Kituo cha Mabasi Ubungo (UBT) watatozwa Sh150,000.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Enea Mrutu alisema hayo jana alipozungumzia mkakati wa kuendelea kuwaondoa wapiga debe hao kwenye UBT. “Operesheni ya kuwaondoa wapiga debe inaleta matumaini kutokana na baadhi ya wamiliki wa mabasi yaliyopo kituoni hapo kuwapo katika zoezi hilo la kuwaondoa ,”alisema Mrutu.
Mrutu alisema hivi sasa wamiliki wanaowalinda wapiga debe wanatozwa Sh150,000.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Wilson Kabwe aliwataka wananchi kuondoa hofu katika operesheni hiyo, bali watoe ushirikiano zaidi. Alisema kazi ya kuondoa watu kama hao si ya siku moja wala mbili ,hivyo kwa ushirikiano uliopo sasa kwa muda wa wiki mbili hizo wanaweka wakawaondoa kabisa.
Alisema lengo la kueleza kuwa watafanikiwa
linatokana na operesheni hiyo kuwabana wamiliki wa mabasi kituoni hapo
pamoja na askari wa jiji wa kituo kushirikiana na ulinzi uliopo chini ya
Taboa.
No comments:
Post a Comment