Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Christopher Sayi amesema, zaidi ya vijiji 1,300 nchini vitajengewa visima vya maji safi na salama ifikapo mwaka 2014.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Christopher Sayi amesema, zaidi ya vijiji 1,300 nchini vitajengewa visima vya maji safi na salama ifikapo mwaka 2014.
Sayi alisema hayo juzi usiku wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Kimataifa wa kujadili jinsi ya kupunguza hatari ya
upatikanaji wa maji na uendelevu wa huduma hiyo.
“Upatikanaji wa maji mijini unaongezeka na unaridhisha lakini kwa vijijini bado ni tatizo ambapo wizara inahakikisha ifikapo mwaka 2014 zaidi ya vijiji 1,300 katika kila vijiji 10 vitakuwa na visima vya maji,” alisema Mhandisi Sayi.
“Wadau wa sekta binafsi kwa kushirikiana nao uzoefu na mbinu mbalimbali tunaweza kufukia malengo ya huduma ya maji kupatikana kwa wingi na kwa ufanisi,” alisema Sayi.
Naye Balozi wa Ujerumani Nchini, Klaus-Peter
Brandes ambaye nchi yake kupitia Shirika la
Maendeleo la (GIZ) ndio waandaaji wa mkutano huo alisema, wataendelea kujitolea kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa nchi za Ukanda wa Jangwa la Sahara unaimarika.
Maendeleo la (GIZ) ndio waandaaji wa mkutano huo alisema, wataendelea kujitolea kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa nchi za Ukanda wa Jangwa la Sahara unaimarika.
Alisema katika ukanda huo,Tanzania imekuwa
ikionyesha jitihada za kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo
hivyo kuwa mfano kwa nchi za Jangwa hilo.
Awali akiwasilisha mada, Mkurugenzi Mtendaji wa
Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Andrew Kaggwa alisema,
watu wawili kati ya kumi duniani wanakosa huduma ya majisafi na salama.
Kaggwa alisema ndani ya miaka 10 ijayo nchi ndogo
za Ukanda wa Jangwa la Sahara kutakuwa na haja ya kufanya uwekezaji kwa
kila mwaka kwa kutumia dola 15-70 katika pato ili kuboresha miundombinu
ya kuhifadhi huduma ya maji.
No comments:
Post a Comment