Na Mwandishi Wetu
TIMU ya
Sofapaka ya Kenya, inatarajia kuwasili nchini Juni 10, kwa ajili ya kucheza
mechi mbili za kirafiki dhidi ya Yanga na Simba.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Smartsports, George
Wakuganda, amesema kuwa, mechi hizo zitakuwa nzuri kwa timu zote kuwajaribu
wachezaji wapya.
“Hii itakuwa
nafasi nzuri kwa timu zote kuwajaribu wachezaji wao wapya watakao wasajili kwa
ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara,” amesema.
Wakuganda
amesema baada ya Sofapaka kuwasili jijini Dar es Salaam, itacheza mechi yake ya
kwanza Juni 12 dhidi ya Simba, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
“Sofapaka
wataanza kucheza na Simba Juni 12, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam, tunaamini Wekundu wa Msimbazi watatumia nafasi hii kuwaonesha
mashabiki wao vifaa vyao vipya,” amesema.
Mkurugenzi
huyo wa Smartsports, alisema Juni 13, kikosi hicho kutoka Kenya kitashuka tena
uwanjani kuumana na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Afrika Mashariki
(Kombe la Kagame), Yanga.
Amesema
mechi hiyo itakuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa timu hiyo kuwaona wachezaji wao
wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao, Mrisho Ngassa na wengine, wakiwa
wamevaa jezi za rangi ya njano na kijani.
Yanga hivi
karibuni imewatangaza wachezaji wapya wawili, wakitokea Simba, huku Haruna
Niyonzima akiongeza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo.
No comments:
Post a Comment