HATIMAYE taji la Redd’s Miss Mzizima 2013, lililokuwa likiwaniwa
na warembo zaidi ya 15, juzi usiku lilitwaliwa na Shamimu Mohammed
ndani ya ukumbi wa hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Katika fainali hizo zilizokuwa na msisimko wa aina yake, wanyange hao
walikuwa kwenye mchuano mkali, huku wakisindikizwa na bendi ya Twanga
Pepeta, ambapo majaji wa shindano hilo walichuja na kubakia warembo
watano na baadaye Shamimu alitangazwa kunyakua taji hilo.
Kwa ushindi huo, Shamimu alikabidhiwa zawadi ya sofa na fedha taslimu sh 400,000.
Mshindi wa pili, nafasi hiyo ilinyakuliwa na Munira aliyepata sh
300,000 huku mshindi wa pili akiibuka Rehema Mpanda aliyejitwalia sh
200,000.
Warembo wote walioingia tano bora, watashiriki shindano la Redd’s Miss Ilala 2013.
Kwa upande wake, Msemaji wa Kampuni ya Kowack Brothers iliyoratibu
shindano hilo, Aneth Makagua, alishukuru wadhamini kwa kuwaunga mkono,
pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza katika fainali hizo.
Wadhamini wakuu wa shindano hilo ni pamoja na Club Bilicanas, Tesco
Funiture, kinywaji cha Chill Will, Tanzania Daima, CXC Africa, Gogo
Shop, Lakairo Investment, Lamada Hotel, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji cha Redd’s na wengineo.
No comments:
Post a Comment