Nina imani kila uliyemchagua kuwa mpenzio ni chaguo la moyo wako hasa
nikizingatia kuna wanawake wengi au wanaume wengi lakini upo na huyo
mwenzio.
Yaweza kuwa mpenzio si wewe wa kwanza kumpenda, huenda yeye
alikupenda kabla yako, pengine uzito wa mdomo wake au desturi ya mila
zetu kuwa mmoja ndiye mwenye uwezo wa kuongea lile linalo msibu juu ya
matamanio ya moyo na mwili.
Kwanza lazima tujue kukaa pamoja au
kuchagua mpenzi ni bahati nasibu unaweza penda pasipo na penzi, wewe
umekwisha na umeoza lakini mwenzio yupo hajali mateso ya moyo wako,
anachojali ni kuufurahisha mwili wake na siyo kufurahisha nafsi yako.
Nina
imani kila atafutaye mpenzi hutafuta wa kufa na kuzikana, wapo
wanaoanza uchumba mpaka ndoa kamili, pia wapo wanaowataka watu kwa ajili
ya kuangalia mwanamke ana nini kutokana na sura, umbile au sauti yake.
Wengine
utanashati wako ‘u-handsome’ ndiyo uliomvutia au hata umbile lako la
kimazoezi nalo limemfanya ajisikie kufanya mapenzi na wewe, na siyo kuwa
anakupenda bali kuna kitu kimemvutia.
Wengine wapo kimaslahi, fedha zinapoisha na mkataba unaisha hapohapo. Wapo wanawake duniani wasiojua dunia inakwenda wapi na nini hatma ya maisha yao, hawa ni wanawake wanaokutana na wanaume baa na kuagana nyumba ya wageni na baada ya hapo hamjuani.

Hawa mwisho wao huwa mbaya, utashangaa mwanamke mzuri kwa
nini haolewi lakini ukisikia sifa zake ni kichefuchefu kitupu, utaambiwa
kila mwanaume mwenye fedha ametia saini kwenye mwili wake.
Ndiyo maana nikawaita viumbe wasiojua dunia ipo wapi na inakwenda wapi na kutojua hatima ya maisha yao.
Wanabakia
simulizi eti enzi zake hoteli gani ya kifahari ambayo hajalala, haya
umelala au mwanaume gani maarufu hajalala naye, nini faida yake? Jibu
hakuna ndiyo maana nikakumbuka neno la masihi kuwa hawajui watendayo.
Asilimia kubwa ya wanawake wazuri au maarufu ndiyo wanaongoza kwa uchafu, wengi wao ni mama huruma wasiojua kumkataa mwanaume mwenye fedha.
Asilimia kubwa ya wanawake wazuri au maarufu ndiyo wanaongoza kwa uchafu, wengi wao ni mama huruma wasiojua kumkataa mwanaume mwenye fedha.
Kwa mfano
mdogo mastaa wetu wa kike au wa kiume wamekuwa na msururu wa wapenzi
kwa vile wengi ni malimbukeni kutokana na kuamini uzuri au umaarufu
walionao ni bahati mbaya.
Wengi hawafahamu kuwa walichonacho ni kitu cha mpito, hawajiulizi katika dunia hii walipita warembo wangapi maarufu? Lakini leo si lolote si chochote, kwa kutumia uzuri na umaarufu vibaya matokeo yake wamekosa thamani katika jamii.

Nafasi uliyoipata itumike kukujenga siyo kukubomoa na thamani ya mwili wako ni kubwa.
Jiepushe kuugawa mwili wako kama pipi kwa sababu tu kila mtu anakutaka wewe, lazima uwe na msimamo ili kujijengea heshima.
Jiepushe kuugawa mwili wako kama pipi kwa sababu tu kila mtu anakutaka wewe, lazima uwe na msimamo ili kujijengea heshima.
No comments:
Post a Comment