WANAWAKE wajasiriamali wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao badala ya kufanya mambo yasiyofaa.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na
Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, katika mkutano wa tano wa
uchumi wa wanawake wajasiriamali.
Akizungumza katika mkutano huo uliondaliwa na Kampuni ya Dare To
Dream alisema: “Ni vizuri wafanyabiashara wakatumia mitandao ya kijamii
ipasavyo katika kutangaza biashara zao sambamba na huduma ya M-pesa
kwa ajili ya kuokoa muda wa kupanga foleni kwenye benki, mwanamke
mjasiriamali akiwa mtumiaji wa huduma hii anakuwa katika hali ya usalama
zaidi kwa fedha zake,” alisema Lyon.
Alisema huduma hiyo hivi sasa imepanuka kiasi cha kutoa huduma zaidi
ya 200, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake wote nchini
kujiunga.
Mkutano huo uliowakutanisha wanawake wajasiriamali uliambatana na
mafunzo mbalimbali ya kukuza biashara pamoja na maonesho ya bidhaa
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment